
LOML | Love Of My Life (171)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:171
Hata Willy alishangaa, ila alificha mshangao wake. Walianza kutoka alipofika mlangoni nilisema βPina thanks, Nakupenda.β
Pina alitabasamu na kusema βRicky, thanks so very Much, I love you.β
Nilitabasamu, hata Willy alitabasamu tu na kisha walitoka na kuniacha natabasamu tu.
Nilizinduliwa na simu ya baba yangu nikapokea haraka na baba alikuwa analalamika βkwanini unaumwa na husemi eenh, kwaninu unafanya hivyo, nakuja hapo na uwe na majibu yangu.β
Nilisema kwa upole βdady please am Sorry.β
Baba yangu alisema βhapana, nakuja hapo.β
Nilitabasamu tu najua baba yangu anavyo nipenda. Ananipenda sana.Ananipenda na kuna muda najua kabisa napendwa sana.
Baada ya Muda rafiki yangu alirudi, alikuwa anatabasamu na kusema βkaka sikuelewi unajua, naomba maelekezo.β
Nilitabasamu na kusema βam falling kaka, nazama kwa mapenzi ya Pina tangu siku ya kwanza nimemuona.
Siku ya ndoa yangu kanisani. Lakini ulinishauri kuipa ndoa yangu nafasi. Nakuhakikishia sijawahi msaliti mke wangu na leo ndiyo mara ya kwanza namwambia ukweli kuwa nampenda. Unamuonaje?β
Alitabasamu na kusema βanaonekana mwanamke makini sana, mzuri sana, halafu mnaendana sana mna vibe fulani hivi mnanishinda hata mimi na mke wangu kifupi mna match.
Lakini kuna jambo sielewi, umesema unampenda mbele ya mkeo, na mama yako huoni kama unakosea kwa maana wewe ni mume wake bado.β