LOML | Love Of My Life (173)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:173
Nilimtazama na kusema β€œbaba usiseme hivyo baba, usifanye hivyo. Wewe ni baba yangu na unajua nakupenda sana. Nilichanganyikiwa tu baba lakini wewe unajua.”

Baba alinitazama na kusema β€œpole sana mwanangu, natamani sana kujua nini kinakusumbua. Unaniambia mambo juu juu pengine ndiyo maana sioni uzito wake. Kwani na mke wako una shida gani. Maana mama yako amekuja nyumbani analalamika sana, anafikia hatua anasema umerogwa sio akili yako.

Unamuacha mke wako mbele ya mchepuko na huyo mchepuko ni mswahili balaa. Anasema amemtukana sana, sielewi mwanangu, sielewi unaweza kunisaidia kuelewa kwanini haya mambo?, anachosema mama yako ni kweli?, na unaonaje tuzungumze na uniambie ukweli wa mambo yalivyo ili nikusaidie kijana wangu.”

Baba yangu alikuwa anazungumza kwa huruma sana. Niliona hilo kwenye macho yangu. Nilimtazama usoni, nikawa nataka kukaa nashindwa hivyo baba alinisaidia. Niliketi vizuri na kisha baada ya hapo nilivuta pumzi na kusema β€œnisamehe sana baba.

Najua kwamba nimekuangusha sana. Nikikuahidi nitakuwa kijana mtulivu na mzuri kwa familia, nilikuahidi kuwa nitakuza familia hii kwasababu najua unavyo penda watoto baba. Lakini nimeshindwa sio na Gabby baba, ndoa yangu na Gabby ni kosa kubwa kwenye maisha yangu.

Imenionesha mambo mengi mabaya ambayo hata sijawahi kuyafikiria kabisa kwenye maisha yangu na ndiyo maana ninataka kuiua.

Baba, mama alichokuambia kuhusu mwanamke mwingine ni kweli na leo hapa ndiyo rasmi mahusiano yameanza, kuhusu kumtukana hapa Pina kamwe hawezi mtukana mama yangu, kamwe hawezi kabisa.

Ni mwanamke mzuri, mchaMungu na anayejitambua bali wao ndiyo walio mtukana kwasababu ni kipofu, kwasababu ni maskini, kwasababu hajavaa kama wao, ni haki hiyo baba?”

Baba aliona nina huzuni, alikaa karibu yangu akanishika mikono kwa upendo na aliniambia β€œnakuelewa sana mwanangu, ninakuelewa mno. Nakuomba sana mwanangu usifanye kosa kubwa zaidi kwenye maisha yako. Sikia mwanangu wewe bado ni mume wa mtu, mwanamke anaweza kugeuza makosa yote wewe ndiyo ukaonekana una matatizo kumbe ni yeye. Kwanini usingejizuia kijana wangu, eenh Ricky baba, kwanini mwanangu?”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

BIKIRA YA BIBI HARUSI FULL

LOML | Love Of My Life FULL

UTAMU WA JAMILA FULL

KIAPO CHA MASIKINI FULL