
LOML | Love Of My Life (175)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:175
Baba aliinuka akaenda mlangoni akarudi akaenda tena akisema βYesu!!, Yesu Kristooo!!, Yesu na Maria,Yesu wa msalabani, Jesus!! Ni nini hiki?, ina maana binti yule ni shetani namna hii, mapenzi yote ya laana anayo yeye.
Huyo sio mwanamke, hafai kabisa, ni pepo, ni jini, ni shetani ni mchawi kabisa. Hatakiwi kukusogelea kabisa, anataka kukua huyu binti. Hafananiii, hafananii hata kidogo. Mungu wanguu naogopa!!, una mfahamu huyo mwanamke mwenzie?β
Huku nalia sana nikimtazama baba nilisema βsana baba, sanaaaa, ni mtu namwamini sana. Sijawahi kuwa na shaka naye, sijawahi kuwa na wasiwasi naye. Nilijua ni mtu wa maana na mtu mwenye akili kumbe hapana. Giana baba, Giana rafiki wa Gabby.β
Baba alichoka, alichoka akisema βdunia imeisha, hiki kizazi cha blueband imekuaje. Binti mzuri mwenye hekima kama yule. Si ameolewa pia yule, Astaghfirullah, Astaghfirullah, Astaghfirullah, Astaghfirullah.β
Baba mpaka kiarabu kilipanda, alinitazama na kuniuliza βmbona ulikuwa husemi mwanangu, eenh ulikuwa husemi kwanini?β
Nililia mwilini mwa baba yangu nikisema βnilijali maisha yenu, heshima yenu, na maisha yetu wote. Niliwasikiliza na kumpa nafasi ili awe bora zaidi baba, ona alivyoniumiza, ameniumiza sana baba naumia na nateseka sana. Sitaki kumuona kabisa, baba nateseka.β
Baba alisema βsitaki hata kumsikia, binti mshenzi sana. Kama nilivyo enda kuomba ndoa yenu. Na sasa nitakuwa mstari wa mbele kuhakikisha ndoa hii inavunjika haraka sana.
Nataka kuona unampa taraka mbele ya macho yangu, hafai kabisa, nitatumia kila njia, kila namna muachane haraka. Anataka kukuua mwanangu na ninaye wewe tu. Msichana mpumbavu sana huyu.
Nilijua mtu ukisoma walau unajitambua. Hata mbwa hafanyi kama yeye, hawapandani wao kwa wao wenye jinsia moja ameanzaje?, anataka kuleta laana kwenye ukoo wetu. Ashindwe kabisa tena asikuguse kabisa.β
Nilimtazama baba na kusema βbaba nashukuru sana, walau unanielewa, unanisikiliza na kujali hisia zangu. Baba mambo mengi unanifanyia bila wewe sijui hata ingekuwaje. My hero, nakupenda sana baba yangu.β