
LOML | Love Of My Life (178)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:178
Baba alitabasamu ba kusema βnimetokea kukuhurumia sana, na kwasababu kijana wangu anakupenda nami nakuona kama binti yangu. Nitapambana upone. Endeleeni mimi natoka nitarudi.β
Baba yangy alionekana kampenda sana Pina. Umewahi kwenda mahali tu unapendwa mpaka unashangaa ndiyo Pina sasa. Alifurahi akanikumbatia akisema βbaba yako ni mzuri sana, ana maanisha nitapona kweli?β
Nilitabasamu na kusema βbaba huwa hatanii hapo usikute kaenda zake kitengo cha macho.β
Pina alisema βmiaka minne hiyo ilikuwa Milion 7 kunitibia sasa si itakuwa gharama sana.β
Nilitamani kucheka maana kwa baba hiyo hata sio pesa. Nilimwambia βmuamini tu, utaona hata iwe 20 baba akikuahidi lazima atimize.β
Alinitazama na kusema βuna bahati sana, kuwa na baba kama huyu niamini, ila mke sasa mkali kama nini?β
Tukacheka, Pina aliendelea kusema βsasa natamani sana kukuona, natamani kuona namna ulivyo mzuri wa moyo na uso wako, natamani kumuona kijana wangu akikua, na sasa baba yako malaika wangu mwingine ambaye anataka kuja kukusaidia, na bado ninaye bibi.
Mungu sikia maombi yangu, maombi yangu ni kuona naona Mungu ananijibu kwa namna ambayo sikudhani kabisa.β