
LOML | Love Of My Life (180)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:180
Tukacheka, nakumbuka nilimshika uso wake na kusema βukiwa na furaha kama hivu una kuwa mzuri zaidi, unanivutia zaidi mpenzi wangu. Pina kama kuna mtu hajawahi kukuambia ulivyo mzuri. Sidhani kama amekutana na watu wazuri duniani.
Binafsi sina mfano wa kutosha kuelezea namna ulivyo mzuri. Wewe ni mzuri sana, ni kazuri mno. Unanichanganya, nakupenda sana.β
Pina alitabasamu na kuniambia akinipapasapapasa usoni, βhisia zangu hazidanganyi, sijawahi kukutana na mwanaume mzuri kwenye hii dunia kukushinda wewe. Sina macho lakini nakufahamu tayari. Wewe ni bonge la handsome na macho yako makubwa hayo nakupenda.β
Nilicheka na kusema βumejuaje nina macho eneh, umejuaje,β
Alitabasamu na kushika, na kusema βkwa kugusa, kushika, kuhisi najua vitu vingi. Wewe ni mwanaume mwenye mvuto Ricky, una macho mazuri yaliyo jaa huruma na upendo. Haya kula sasa..β
Nilitabasamu na kusema βsasa mbona hujamalizia My smiley!!!β
Alitabasamu na kusema βMy fortune.β
Nilitabasamu na kusema βMy fate.β
Kisha nikawa namtazama vile anatabasamu, nikachukua kijiko na kumlisha pia, alinishukuru na nikawa naendelea kulishwa huku nikimuelezea nimeongea na baba kuhusu Gabby na namna amepokea. Pina alisema kwa upole βpole sana Ricky, haujachelewa bado na sitaki kuingilia sana suala hili. Lakini nipo hapa na wewe ukinihitaji nipo hapa.β
Nilitabasamu na kusema βnajua ni ngumu kunielewa, lakini umenipa sababu ya kuwepo, sababu ya kupumua kwa nguvu zangu zote na kupambania maisha yangu. Nakupenda.β
Nilimshika mashavu na kumbusu, nikawa namtazama na wakati huo Willy na mke wake wanaingia, na nikatabasamu nikisema βkaribu sana shemeji.β