LOML | Love Of My Life (181)

๐‹๐Ž๐Œ๐‹ (๐‘ณ๐’๐’—๐’† ๐’๐’‡ ๐’Ž๐’š ๐’๐’Š๐’‡๐’†) โฃ๏ธ:181
Shemeji yangu alitabasamu na kusema โ€œpole sana shemeji yangu.โ€
Willy alicheka na kusema โ€œshemeji yako hapo roho kwatu alijua sijui nashinda wapi usiku kapambana aje haya sasa mgonjwa huyu hapa.โ€

Tulicheka tu, kisha nilimtambulisha Pina, mke wa Willy hanaga maneno yeye ni heshima tu. Tulikuwa tunacheka pale hata baba aliingia. Walimsalimia na kisha alisema โ€œMwanangu, unaweza kunifuata mara moja?โ€

Tulitazamana, kisha baba alisema โ€œPina binti yangu unaweza kunifuata?โ€
Nilitabasamu na kusema โ€œnilikuambia mimi, sasa si umeona.โ€
Pina aliinuka, baba yangy alimshika mkono na huku Willy akiniuliza โ€œwanaenda wapi tena?โ€

Nilitabasamu na kusema โ€œwapi kama sio kwa dokta wa macho. Si unamjua baba Ricky?โ€
Willy alisema โ€œwee usinambie, mzee wako ana upendo sana lakini na hapo tena roho ya kijana wake. Maskini Pina haamini pale.โ€

Nilitabasamu tu, huku shemeji akisema โ€œnafurahi kuona unaendelea vizuri shemeji yangu.โ€
Nilitabasamu na kusema โ€œnashukuru kwa upendo na chakula. Ubarikiwe sana.โ€
Alitabasamu tu, na kisha alisema โ€œna leo nimebeba ila nishawahiwa.โ€

Tukacheka huku Willy akisema โ€œtutakula wenyewe kwanza mimi mwenyewe nina njaa.โ€
Mke wake alisema โ€œbaba huna aibu wewe cha mgonjwa ujue.โ€
Basi tulicheka sana.

Muda ulizidi kwenda baba na Pina hawakurudi hata Willy na mke wake waliaga na nikabaki peke yangu. Baada ya muda walirudi, Pina hakuonekana kuwa na furaha. Nikauliza โ€œbaba kuna nini tena?โ€

Baba aliniambia โ€œusijali mwanangu, dokta wamemchek, kadri anavyozidi kukaa na hali hii bila kutibiwa anazidi kuharibikiwa. Lakini wameshauri twende India. Na nimeona ni kitu kizuri.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

KIAPO CHA MASIKINI FULL

SHEM MI NATAKA FULL

CHAGUO LA MOYO FULL

SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? FULL