LOML | Love Of My Life (182)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:182
Na naahidi tena kuwa utakapo maliza mambo yako, wewe na yeye mtaenda huko na ataona tena bila kujali daktari wanasema nini. Ondoa hofu binti yangu hakuna gumu chini ya jua.

Wakati mwenzako anashughulika na mambo yake mimi nitawatafutia utaratibu mzuri na nitaweka sawa kila kitu mtaenda huko.”

Pina alimkunbatia baba kwa nguvu, alilia akisema “nashukuru sana baba, Mungu akubariki sana.”

Baba alikuwa hawezi hata kusema kitu, alikuja na kunikumbatia kwa nguvu, nilifurahi sana. Baba alinitazama na kusema “natoka wanangu, tutawasiliana sawa.”

Nilisema kwa upole “baba yangu kipenzi, nashukuru kwa kila kitu. Wewe ni baba bora sana kwangu.”
Baba alitabasamu na kusema “nakupenda sana mwanangu. Napenda furaha yako.”

Nilitabasamu, na baba aliendelea “anything for you my boy!!”
Nilitabasamu na kusema “gat you dady!!”
Alitabasamu na kutoka akisema “Pina mlinde huyo narudi tena.”

Pina alitabasamu na kisha alianza kulia akisema “namshukuru sana Mungu kwa kunikutanisha na wewe. Kila kitu kinazo sababu, na kumbe ili mimi kupona ilikuwa ni lazima niwe na wewe. Ricky, nashindwa kujizuia, nashindwa kabisa. Baba yako, hakuna mtu amewahi nitendea kama yeye au wewe. Ninyi ni watu wa sayari gani.”

Nilitabasamu nikisema “Pina tulia kwanza sawa mumy, mambo madogo nakuahidi kesho tunatoka hapa ili nikaanze kushughulikia haya na kisha utaona lazima.”

Pina alilia akisema “naikumbuka sana ile siku Ricky, naikumbuka nilimuacha mwanangu, na kwenda kupika. Huku napika na mshono wangu wenye maumivu, mtoto analia na mimi nahangaika na jiko.Nilipika, nilipika mpaka nikamaliza.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata