LOML | Love Of My Life (184)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:184
Nilijisikia ovyo, niliona hii nafasi nikitoka sitarudi. Nilitoka nikatafuta usafiri, nikabeba vitu muhimu kwa pochi yangu na mwanangu. Niliingia kwa bajaji, nilikuwa nalia kuanzia natoka pale nyumbani mpaka hospitali.

Huku moyoni nahangaika sana kwanini huyo mzazi mwenzake ana shinda pale nyumbani au kuna uhusiano gani na mume wangu. Nakuwa sielewi kwanini?”

Nilifika hospitali, mpaka nafika pale, kila mtu yupo na ndugu yake kasoro mimi tu. Nilijisikia vibaya. Niliingia mpaka ndani nesi akaniambia β€œmtoto muachie ndugu yako.”
Nilijibu kwa upole β€œnimekuja peke yangu.”

Nesi alishangaa akisema β€œpeke yako, hata mumeo hayupo haya sasa huyo mtoto tunafanyaje. Mlaze hapo kitandani mlale wote maana hakuna mtu wa kukushikia.”

Nilitii tu, niliamua kumlaza mtoto wangu na kisha nilifanyiwa dressing na baada ya hapo nikachukua mwanangu na kuondoka zangu na safari ilikuwa kwangu. Nilipofika nilichukua funguo mahali huwa tunaficha na kuingia ndani. Nikampigia mume wangu apitie vitu vyangu.

Akaniuliza β€œkwani kuna nini?”
Nilijikaza na kusema β€œnajisikia vizuri tu mume wangu sioni haja ya kuwa kule kuwasumbua.”
Mume wangu aliniambia β€œnikirudi tutazungumza.”

Kweli jioni mume wangu alirudi na mizigo, nilimpokea mara simu ya mama iliita. Mume wangu aliweka loud, nikawa namsikia mama anasema β€œnilikuambia huyo mkeo jeuri sana. Hajaaga mtu yeyote anaondoka kwamba sisis tunamtesa au ni kitu gani.

Mwanamke mchoyo sana huyo, ana roho mbaya sijui hata umemtoa wapi, eenh kwanini mwanamke mbinafsi namna hiyo.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata