LOML | Love Of My Life (185)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:185
Machozi yalinitoka, niliumia sana, mume wangu alitoa loud na kuondoka pale kwenda kuzungumza na mama yake. Nilibaki natokwa na machozi.

Baada ya mume wangu kurudi nilimuuliza β€œkwanini mama yako hanipendi namna hii, sijui hata nimekosea wapi aniambie niombe msamaha.”
Mume wangu aliondoka na kusema β€œna wewe kwanini umeondoka eenh, ungesubiri hata wiki walau.”

Niliita kwa huruma β€œIsack mume wangu, nitakaa vipi sehemu mzazi mwenzako yupo hapo siku nzima. Na familia yako hawanipendi mimi. Kila kitu najifanyia, kila kitu yaani.”

Mume wangu alinitazama na kusema β€œsasa mzazi mwenzangu anakuhusu nini. Na unasema kila kitu unajifanyia. Ina maana mama yangu anavyosema amekufanyia kila kitu kwa upendo ni muongo. Unamsingizia mama yangu.

Upendo wote anao kupa leo hii unamuona muongo. Aliacha mambo yake akawa anakuja hapa kwaajili yako leo akufanyie ukatili.

Sikuwa najua una roho mbaya sana mpaka kwa mama yangu kweli, mama alikuwa sahihi ona sasa una msingizia mama yangu mzazi.”

Nilishindwa zuia machozi nilijikuta nasema β€œMume wangu, Isack unanifahamu vizuri unajua siwezi kufanya hivyo kwanini?”
Isack alinitazama akanisonya na kuondoka zake.Nililia zaidi kuona hata mume wangu anaona mimi ni kama mama yake anavyosema. Niliumia sana, usiku huu nililia mno. Roho yangu iliniuma sana, niliumia kupita kiasi.

Nilishinda nalia asubuhi niliamka naumwa sana macho yangu, yalivimba nilijua ni kwasababu nimelia sana. Niliendelea na mambo yangu huku nikimpigia sana simu mume wangu bila mafanikio. Mume wangu hakuwa hata anapokea simu yangu. Ilipita hii siku nilimsubiri mume wangu sana. Hakurudi nyumbani kabisa. Pamoja na jumbe za kuomba msamaha wakati hata sikuwa nimekosea lakini mume wangu hakurudi. Niliumia sana.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata