
LOML | Love Of My Life (188)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:188
Bibi aliniambia βsitaki nikulaumu mwanangu ila hiyo familia umeingia hakuna familia hapo. Sijui kama ni watu wazuri sina imani nao kabisa.Sasa ndiyo wamefanya nini kwa mtoto.Naomba mpigie huyo wa maombi leoleo tuone itakuaje.β
Basi niliheshimu mawazo ya bibi yangu, mida ya saa mbili nilimpigia mtu wa maombi nikamuelezea namna nimepata namba yake. Tulianza kusali kupitia simu. Kuna watu wanajua sana kuomba, niliomba naye karibia lisaa na nusu, mtoto wangu alikuwa ametulia kama anaelewa vile.
Nilishangaa, baada ya kumaliza nikatuma na sadaka nikisema βMungu kama hii familia ina lengo baya na mimi nitoe hofu, nikumbatie na unitenge nayo. Naomba nisaidie Mungu wangu. Hii sadaka ikanipe majibu ya maswali yangu yote.βNikatuma ile sadaka.
Δ°le usiku mtoto alilala sana, nilikuwa namshangaa Mungu. Na mimi nikalala, nilipo lala nikaota nipo nyumbani kwa Wakwe zangu. Mama mkwe wangu ananiuliza βhivi mwanangu, mjukuu wangu anaendeleaje?β
Nilimtazama, nikamwambia βanaendelea vizuri.β
Akaguna na kusema βkumbe yupo, mimi nilidhani hata hayupo, Mungu mkubwa sana.β
Nilimtazama tu, na Kisha nilisema βnisikie vizuri wewe mama, naomba nisikilize kuanzia leo, mtoto wangu hatoitwa hilo jina unaloita. Na utakaa naye mbali na kama chochote kibaya kikimkuta mtoto wangu. Wewe ndiyo sababu utamla nyama yake.β
Nilishtuka, ile nimeshtula simu yangu iliita, kutazama alikuwa ni mama mkwe. Nilishangaa, nilipokea simu na kusema βshikamoo!!β
Akaniambia βmkwe wangu jeuri huyo mjukuu wangu anaendeleaje.β