LOML | Love Of My Life (189)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:189
Hapa sasa ndiyo nilijifunza Kumbe haya majina ni muhimu kujua chanzo chake, nilijikaza na kusema β€œmama hilo jina La mtoto silitumii na hata tumia hilo jina. Mwanangu anaitwa Samwel. Na anaendelea vizuri kabisa.”

Mama alisema kwa kiburi β€œhivi wewe binti una shida gani, unajikuta Nani wewe, unajitia mjanja na ndiyo maana ndoa yako Ina kushinda, sasa utaona utaishia wapi.”

Nilimjibu β€œkitu pekee najua sijawahi kuwakosea, na sitawakosea. Mtakaa mbali na mimi kama nilivyokaa mbali na ninyi. Mwanangu mumuache.”
Mama huyu akaniuliza β€œUnataka kusema mimi mchawi ndiyo naroga mwanao aumwe si ndiyo?”

Mimi nilikata simu, kumuangalia mtoto bado hata choo hapati. Nilimpigia bibi na kumsimulia bibi aliniambia β€œachana nao mjukuu wangu usigombane nao. Kama mwanaume hakutaki basi tulia mwanangu tunza mtoto utafute kazi.”
Haikuwa rahisi Ila niliitikia tu.

Ninakumbuka lisaa lilipita mume wangu alinipigia anafoka β€œhivi wewe mwanamke unachanganyikiwa unapata wapi ujasiri wa kumuita mama yangu mchawi, unapata wapi hizo nguvu eenh, una akili wewe, una akili, sasa una washa moto ambao hauwezi kuuzima.”

Niliguna tu, niliona nimejichanganya mwanaume niliamini ananipenda na yeye anasikiliza kila kitu cha mama yake hajali kuhusu mimi kabisa. Niliendelea na mambo yangu moyoni nikiomba Mungu sana mwanangu ajisaidie maana anateseka.

Muda wa saa moja mwanangu alikuwa anahangaika sana. Alikuwa anajikamua. Ilinibidi nimpigie bibi yangu, nikamwambia Hali halisi ya mtoto na muda wote mimi hapo macho yanavimba hayapati nafuu Ila akili yote kwa mtoto.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

BIOLOGY TEACHER FULL

UTAMU WA JAMILA FULL

SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? FULL