
LOML | Love Of My Life (192)

ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:192
Bibi yangu ndiyo alikuwa msaada kuanzia pale, maumivu, mateso ya kuomba omba, kunyanyasika, kukubali hali mpya kutoka kwa mwanaume niliyempenda haikuwa rahisi lakini kilinifanya niwe karibu sana na Mungu.
Tangu hapo sijawahi hata kujua maisha Yao, wala kusikia habari zao. Naamini Mungu amewapa wanacho stahili. Yapo Mengi Ila nimeamua kufupisha walau ujue nilivyoishi kwa mateso.
Kuna muda nasali sijui nitapata muujiza au natakiwa kupona hospitali. Δ°mani yangu inaniambia nitapona lakini sielewi, mwanangu Nilimtazama naishia kusema asante Mungu. β
Nilimuhurumia nikisema βinatosha Pina, inatosha unajua tunatakiwa kufurahi. Tuunganishe haya maumivu tuwe kitu kimoja. Stop weeping, Nakupenda sana. Sahau hayo yote ulikuwa lazΔ±ma upite ili umjue Mungu namna hii. Nakuomba usilie.β
Pina alinikumbatia na mimi nilimkumbatia. Ulikuwa usiku mzuri sana, hata baba yangu hakurudi hapa. Na asubuhi nilipoamka, Pina alikuwa amenishika mkono anasali, alipomaliza nilisema βAmen.β
Alitabasamu na kusema βNaona leo umeamka vizuri. Good morning handsome wangu, Mimi naomba nikuache Mara moja nitarudi Baada ya muda nikamsaidie bibi kazi.β
Nilimwambia kWa upole βSubiri nikuitie dereva.β
Aliniambia kWa upole βHapana mpenzi usimsumbue nitafika.β
Nilikataa na kusema βHaiwezekani.β
Nilichukua simu na kumpigia Dereva, kweli Baada ya muda alimfuata na mimi nilikuwa hapa. Siku hii niliamka vizuri, hata nilimuomba dokta nitoke.
Nakumbuka niliambiwa nisubiri nikawa tu nakumbuka hadithi ya Pina najisikia vibaya wakati kuna wanawake wajinga Kumbe na wanaume pia ni wengi. Baba alinipigia, akaniuliza Hali yangu nikamuelezea Nimeomba kutoka.

