
LOML | Love Of My Life (194)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:194
Nakumbuka nilimwambia dereva amfuate Pina na mimi nitaenda nyumbani na pikipiki. Ikawa hivyo, nilichelewa chelewa nyumbani. Baada ya muda niliondoka mpaka nyumbani. Nilipofika nilikuta mama babuu akiwa jikoni. Alifurahi sana kuniona hata aliniambia “unaendeleaje Boss, Madam aliniambia unaumwa.”
Nilishangaa na kuuliza “Gabby yupo hapa?”
Mama babuu alinijibu “ndiyo yupo hapa.”
Nilijikuta kichaa kinanipanda, niliita kwa nguvu “Gabby!!, Gabbbbbyyyy!!, Gabby!!”
Gabby alinifuata mbio mbio akisema “welcome back home bedo.”
Nilipata hasira, nilibadilisha uso wangu na kumuuliza “unatafuta nini hapa, niliposema sikutaki hukunielewa. Ingia huko ndani na utoe takataka zako zote.”
Gabby alinitazama akisema “mume wangu, usiwe hivyo tafadhali, nisikilize.”
Nilipiga hatua nikatembea mpaka chumbani nikatoa nguo kabatini na kumuwekea kwa sanduku nikiwa na hasira. Nikaweka karibia sanduku kubwa tatu. Na Kisha niliita “mama Babuuu!!, mama Babuu!!.”
Alikuja mbio mbio, nikasema “mama babuu, toa hızı begi nje. Upo hürü kufanya kazi hapa Ila kama unataka kuungana na shetani huyu ondoka naye.”
Gabby alisema kwa huruma “unanifukuza, hii nyumba ni yetu sote.”
Nilicheka nikisema “una kichaa, hii nyumba nilipewa na baba yangu sio baba yako unanielewa sijui. Hakuna kitu tulichofanya pamoja kama unataka pesa sema.”
Nikawa namtolea begi mpaka sebuleni, alisema “mimi nakutaka wewe sitaki chochote, tuishi wote mpenzi.”
Alinisogelea na kutaka kunibusu, nilimsukuma akaangukia huko na ndiyo Pina alikuwa anaingia na mimi kusema “shenzi wa tabia, wewe Nani unataka kunigusa mimi, huna haki hiyo kamwe na hata ukiniona kaa mbali na mimi unanielewa.”
Nilisikia Gabby akisema “Dadie please.”
Muda huo Pina, alikuwa anatafuta njia ya kuja kwangu na kusema “baby, kitu gani kinaendelea hapa?”
Nilimshika mkono na kusema “nisamehe mpenzi umefika nyumbani unakuta nagombana.”

