
LOML | Love Of My Life (196)

ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:196
Sikuwa hata naelewa, nilihama duniani, nilihamia dunia ya peke yangu. Hapa sasa ndiyo nilikuwa nabusu, nambusu mwanamke ambaye nampenda, mwanamke ambaye ndiyo maisha yangu, yeye ndiyo mpenzi wa maisha yangu, love of my life (Loml).
Akili, moyo vyote vipo hapa. Kumbe ukipenda unakuwa kipofu huoni kingine zaidi ya kufafa moyo na hisia zako, ukipenda unakuwa kiziwi husikii kitu zaidi ya Mpenzi wa maisha yako na sauti yake tamu ikikumbembeleza.
Niseme nini, nikuambie nini, sikuwahi kujisikia namna nimejisikia wakati huu ninapo mbusu huyu mwanamke wa maisha yangu. Pina ni hivi, kila kitu chake ni kizuri. Hapa sijajali ameavaa nini, afanana vipi ninacho kiona kwake ni mzuri. Ni mzuri nashindwa kuelezea.
Natamani kama ungepata nafasi ya kumuona alivyo. Nilikuwa nasema Gabby ana mikogo ya kike. Huyu sasa, madeko yake yanaendana na alivyo, akideka mwanaume unasema mpenzi wangu kadeka.
Alinishika vizuri sana. Halafu wakati huo tulisikia miguno ya koo. Hii ndiyo ilitukumbusha tupo dunia ya wapiga kelele na watu wasiopenda kuona watu wanapendana. Alikuwa ni mama babuuu.
Nilimuachia mpenzi wangu nikimtazama na kutabasamu, halafu nilimkumbatia. Vile akiwa mwilini mwangu jamani, anaonekana vizuri sana. Nilimtazama mama babuu na kusema βUmechagua kubaki hapa?β
Alitabasamu na kusema βnimeamua kuanza maisha yangu upya nikiwa hapa kwaajili yangu na familia yanguβ
Nilitabasamu na kusema βkumbuka mimi ni boss wako, ukiweza uaminifu tutawezana tofauti na hapo bora uondoke. Maisha yangu hayamuhusu Gabby, habari zangu hazimuhusu kabisa.β
Alinitazama na kusema βnakuelewa boss, hata yeye hataki kuniona kabisa kwasababu nimekuchagua zidi yako.β

