
LOML | Love Of My Life (199)

ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:199
Ninakupenda sana, niliposeme wewe ni My fortune, My Fate, and Smiley i meant, na nitasema tena hapa ujue namna gani nakupenda. Wewe ni Hatima yangu Ricky, ninakupenda na ninakupenda na kila kitu changu. Kila kiungo cha moyo wangu kimeitikia penzi lako. Wewe ni wangu Ricky, siwezi kukaa mbali na wewe, siwezi.β
Nilitabasamu, sijui labda ni maneno ya kawaida lakini akiongea huyu mwanamke, akizungumza kila kiungo unachojua wewe. Kinahisi raha, mwili unanisisimuka kwa raha. Raha zinapitiliza mimi. Mwanamke anaongea kwa utulivu, mwanamke anakusifia, anakuambia kila kiungo chake, kimeitikia penzi langu sasa naacha vipi kuweweseka.
Nilimfuta machozi yake na kisha na mimi nilisema βwewe ni mwanamke mzuri ajabu. Sijawahi kuona mwanamke mwenye mvuto namna ulivyo kipenzi changu. Tangu nimekuona ile siku kanisani, sijawahi kupata utulivu.
Nilifanya kila kitu kukuondoa akilini kwangu lakini ndiyo kwanza ulizidi kunifanya nikufuate umbali wote huu. Kitu sijutii ni kukuona wewe. Tabasamu lako ni maisha yangu yote mpenzi, ukitabasamu napata sababu ya kupumua tena na tena na tena na tena.
Napenda sana ukitabasamu ukiwa na mimi, tabasamu, tabasamu kwa kila namna, tabasamu namna unaweza na sitamani kukuona unalia. Hakikisha ukitokwa machozi mama, yanakuwa machozi ya raha, machozi ya furaha, machozi ambayo yatafanya tufurahie maisha yetu yote.
Ndiyo Pina, wewe ni wa pekee, nakupenda jinsi ulivyo, sijali kuhusu macho yako kipenzi bali moyo wako. Naupenda sana moyo wako, napenda sana uhalisia wako, napenda sana ongea yako, napenda zaidi unaposema mimi ni hatima yako.
Najua ni ngumu kunielewa, wewe ni hatima yangu mimi, wewe ni msichana wa maisha yangu, mpenzi wa moyo wangu, mpenzi wa maisha yangu. Sifanyi chochote bila Pina kwenye akili yangu. Hata wewe si unaona unavyonichanganya cha madeko wangu.β
Pina alicheka, na kisha niliinuka na kukaa karibu yake. Halafu Pina alisema βkabla sijaendelea, unatakiwa kujua kudeka ni sehemu ya maisha yangu na nimepata mahali nadekezwa basi mpenzi mimi kuacha kudeka nipeleke mahakamani na ujue nitahukumiwa maisha maana siwezi kuacha, siwezi .β

