
LOML | Love Of My Life (200)

๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ:200
Nikacheka nikisema โdeka tu mama, deka nikudekeze.โ
Pina alinitazama na kusema โsasa my smiley, sasa mimi hapa, sasa, sasa zawadi yangu mimi hapa ipo wapi Ricky wangu.โ
Vile namtazama, kuna mtu ukiwa unadeka unaonekana kama katoto kadogo halafu kuna mwingine kama anashindana na mwingine ana igiza kabisa na mwingine anachekesha.
Sasa huyu wangu akideka kama hivi mimi najikuta meno 32 yote yanakuwa nje kwa kutabasamu na furaha.
Niliinuka na kusema โnisubiri kipenzi nakuja.โ
Nilitembea kuelekea chumbani. Nilifika na kukuta wanaendelea na kazi huku mama Babuu akisema โnamalizia nikaandae kwanza chumba chako kisha huku nitaendelea mdogo mdogo.โ
Nilitabasamu na kusema โnashukuru sana.โ
Mama Babuu alitabasamu na kusema โhongera sana Boss, nimefurahi sana kwa maamuzi yako. Nakutakia kila la heri. Uwe mwenye furaha siku zote.โ
Nilitabasamu na kusema โnashukuru sana.โ
Nilianza kuondoka zangu. Nilifika mlangoni, nilisikia mama Babuu akisema โni mzuri sana, ni mzuri. Nimempenda sana.โ
Nilitabasamu tu na kisha niliendelea na safari. Nilipofika sebuleni, nilikuta Pina amepiga magoti pale nilikuwa nimemuacha na alikuwa ana sali. Nilitabasamu na kukaa kimya. Alitumia muda kidogo na kisha aliniambia โnajua upo hapa Ricky.โ
Nilitabasamu na kusema โsiwezi shindana na hisia zako mama.โ
Alicheka na kusema โunajua ni mbali kiasi huku, ina maana kule ulikuwa unakuja kwaajili yangu.โ
Nilitabasamu na kusema โkiukweli kabisa kwanza ulinivutia sana, na kila ulichofanya kilinivutia. Ndiyo maana nilikuomba yale maombi.
Niliyapenda sana na wakati ule nilikuwa nimevunjika sana moyo wangu. Kupitia wewe na Mungu, nilizidi kuvutiwa kumjua Mungu ingawa bado sijafika kiwango kikubwa. Nakuhakikishia.
Nilikuwa najua kuhusu kanisani, Mungu, na maisha ya kuhudhuria ibada lakini sio kama Baada ya haya yote. Nimekuwa karibu zaidi na Mungu. Vipi wewe, naona kanisani ni mbali zaidi, kwanini pale.โ

