
LOML | Love Of My Life (203)

ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:203
Pina alicheka tu huku akikaa vizuri, nilikuwa namtazama vile anacheka. Unajua naona kama nakuwa mtoto, namna ananifanya nakuwa na furaha naona sio mimi wa hana au juzi ni kama mtu mwingine.
Mimi nacheka Kama sitacheka tena. Kila kitu kilikuwa ni kizuri sana. BaΕΔ± Pina aliniuliza tena kuhusu dawa, niliinuka na kuzifuata, Kisha niliita mama Babuu kwaajili ya maji na Baada ya kunywa tu dawa ndiyo Kwisha habari yangu. Nachoka zaidi hivyo nikalala huku Pina akiwa pale ananitazama.Hata usingizi ulinichukua kabisa.
Sijui ni muda Gani alitoka hapa au alirudi Ila ninachojua nililala kwa masaa mawili hivi ndiyo niliamka. Baada ya kuamka nilimuona akiwa amelala pembeni yangu pia.
Nilimtazama tu na nikawa nimesogea karibu yake zaidi na kuanza kupapasa nywele zake za twende kilioni zilizo sukwa vizuri kabisa, Kisha nyusi zake na midomo, Mara pua namgusa hapa na pale naangalia namna Mungu alivyo Fundi wa kufinyanga watu wake. Pina ni mzuri sana, ana nichanganya na vitu vingi mpaka sijui hata niongelee kitu gani.
Aliamka akisema βina maana hata nesi nimelala sasa Nani atamuamsha mgonjwa?β
Nilicheka nikisema βsi ndiyo hapo sasa.β
Wote tuliamka, akanipapasa na kuniuliza βunajisikiaje mpenzi?β
Nilitabasamu na kusema βNapenda unavyo hali kuhusu namna ninajisikia. Ninajisikia vibaya, kuchoka, kichefuchefu hivi sijielewi yaani.β
Aliniambia kWa upole βni njaa, unatakiwa kula na ushibe vizuri.β
Nilitabasamu na kusema βhakika, kwasababu natakiwa kuamka vizuri kabisa ili nianze mchakato wa maisha yangu mapya vizuri kabisa.Inuka tukale pamoja mpenzi wangu.β
Tuliinuka, na mimi ndiyo nilimshikilia mkono na kumuongoza njia. Tulifika mpaka sehemu ya kupata chakula tuliketi. Mama Babuu ndiye aliye tuandalia chakula, hapo mimi nikiwa karibu na Pina wangu. Chakula kilikuwa kinanukia sana. Hata nilisema βkinanukia sana.β

