
LOML | Love Of My Life (205)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:205
Pina alitabasamu na Kisha alisema “mama!!, tafadhali mimi naomba niite tu Pina!!, ndiyo napenda zaidi.”
Nilitabasamu na Kisha nilisema “Au muite mama Ricky hapo vipi si jina zuri zaidi?”
Tulitazamana na kujikuta tunacheka sana. tulicheka huku Pina akisema “huna akili kabisa, huna akili.”
Wakati anasema hivyo mlango ulikuwa unagongwa, mama Babuu alienda kufungua. Alikuwa ni baba yangu, baba alipofika alisema “kumbe mimi mkulima mzuri, mwanangu share yangu ipo hapo.”
Nilicheka nikisema “baba huwezi kukosa chakula ukiwa kwa mwanao.”
Baba alitabasamu na nilisimama kumkumbatia, Pina alisimama pia na kusema “Shikamoo baba!!”
Baba aliitikia na kusema “nimefurahi sana kukuona hapa binti yangu.”
Pina alitabasamu, baba akaniuliza maendeleo yangu basi nikamuelekeza namna ninajisikia wakati mwingine sawa na wakati mwingine ovyo.
Na niliongeza “Yote kwa yote Namshukuru sana Pina. Amekuwa msaada sana kwangu. Yupo na mimi kila wakati kunikumbusha dawa, namna ya kujitunza na kula.”
Baba alitabasamu, nilimtazama na kusema “eenh mama anaendeleaje?”
Baba alisema “unajua mama yako, bado anaona Yule mchawi ndiyo mwanamke mzuri. Laiti angejua kuwa ni mashine ile ya kusaga na kukoboa angekaa mbali kabisa.”
Tulijikuta tunatazamana na kucheka sana, baba alisema “mnisamehe wanangu, nimechukia sana.”
Baba alinitazama na kusema “hapa ninavyo kuambia mama yako ameenda kwao Gabby. Nasikia Gabby kawaelezea kwao kuwa una mpenzi mpya na humtaki yeye kısa huyo mpenzi.”
Mimi nilimtazama Pina, akawa anatabasamu tu. Mama Babuu yeye alikuwa ana andaa chakula cha baba. Kisha alisema “nashukuru sana kwa chakula kizuri Pina. Ubarikiwe Ila uzingatie tulivyo zungumza.”

