
LOML | Love Of My Life (210)

๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ:210
Shemeji yangu huyu alisema โMungu wangu, haipaswi kuwa hivi kabisa, haitakiwi kuwa hivi sisi ni walezi wa ndoa yenu. Lazฤฑma kuimarisha uhusiano wetu.โ
Nilimtazama na kusema โnimemaliza shemeji yangu. Kama kuna suala kingine kuhusiana na jambo lingine ni sawa. Lakini Kama ni kuhusu mumeo sitamzungumzia tena.โ
Alinitazama tu na kusema โnatamani kujua amefanya nini hata imekuwa hivi.โ
Nilitabasamu na kusema โatakuelezea tu. Ni mume wako, akikuambia uongo utajua, akikuambia ukweli utajua. Lakini kwa kukusaidia kamwe usimwambid ulikuja kwangu. Kwasababu mumeo ni mtu smart.โ
Nilitamani hata kumdadavulia kitu lakini ndani yangu nilikuwa nasikia sauti โacha usifanye hivyo, usifanye hivyo.โ
Alinishangaa tu, mimi nilisema โshemeji yangu, nahitaji kupumzika sasa. Wewe kuwa huru hapa ni nyumbani.โ
Alinitazama na kusema โasante sana shemeji, wacha tu mimi niende. Naona hata haupo vizuri unajichanganya. Mimi nakwenda sasa.โ
Nilitabasamu na kusema โuwe na siku njema Shemeji. Wasalimie sana watoto.โ
Alinitazama na mimi sikujali, nilianza kutembea taratibu kuelekea chumbani. Ni wazi alinitazama mpaka nilipo potea kwake maana sikusikia mlango wa sebuleni ukifunguliwa.
Nilifika mpaka chumbani, nilikuta mtoto mzuri amelala namna fulani hivi eenh, kalalia tumbo halafu kuna namna kamguu kakunja. Gauni yake kuna namna imepanda kidogo na kufanya sehemu za mwili wake kidogo kuonekana.
Nikawa ninamsaili tu mtoto mzuri. Nikiwa hapo nilikumbuka hata simu ya Gabriella ipo kwangu tayari. Nilitamani kufungua tena, lakini niliona haina hata maana. Nilijikausha tu.
Nikisema โinatakiwa kuondoka humu.Nitajua cha kufanya.โ

