
LOML | Love Of My Life (213)

๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ:213
Kiukweli Hali yangu ilikuwa tete, Ila nitafanyaje sasa, ilikuwa tu ni lazฤฑma nijishikilie Ila natamani hiyo siku ifike, hiki kitanda nilale na mwanamke huyu ninayempenda sana. Naona kabisa sitaamka mimi. Maana hapa tu ninasikia raha ajabu.
Nilimtazama na kusema โasante kwa kuja kwenye maisha yangu Pina. Unanifanya nijisikie amani na furaha muda na wakati wote.โ
Alitabasamu na kusema โuwepo wako kwenye maisha yangu una maana zaidi ya kฤฑla kitu kwenye maisha yangu. Nitafanya kila kitu nisikukose maadam najua wewe ni wangu, unanipenda. Niambie Ricky Unanipenda?โ
Nilitabasamu na kusema โNakupenda mno na nitakupambania.โ
Alitabasamu na kuniambia โkwa Mara ya kwanza napata furaha kwenye maisha yangu. Nakuahidi sitakuacha uende, nitakupigania.โ
Nilicheka, Akacheka pia. Nilimtazama pale ukutani na kusema โwiki hili ratiba yangu itakuwa ngumu kidogo lakini jiandae muda na wakati wowote nitakufuata wewe na Samweli tukatembee kidogo.โ
Alinitazama na kuniuliza โumesema na Samweli?โ
Nilitabasamu nikisema โtuondoke sasa, tunachelewa.โ
Akaniuliza โunaendesha wewe?โ
Nilicheka nikisema โkama unataka nikumwage sawaaaa.โ
Tulicheka, tulikuwa tunasema hivyo kwa maana, kwa maana sikuwa na nguvu bado lakini sio nguvu za kubusu hizo kwenye kumbusu Pina zimejaa.
Baลฤฑ nilichukua na simu ya Gabby nikaweka mfukoni. Sikuwa najali Nani kapiga wala nani kamtafuta sikutaka kuhangaika nayo tena. Tuliingia kwa gari, Yule dereva wangu wa kazini ndiyo ilikuwa aendelee na mimi tu mpaka nikae sawa maana kikawaida napenda kujifanyia mambo yangu mwenyewe. Tulikaa nyuma. Sasa ukimuona Pina ameniegemea, nilikuwa nasikia raha sana.

