LOML | Love Of My Life (214)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:214
Nilitaka niseme kama hujisikii hivi ambavyo mimi nina jisikia na huyu mwanamke başı hupendwi kumbe Kuna watu kwao kuteseka ndiyo mapenzi nyie siwezi waambia lolote.

Unajua kuna wakati ninavyo jisikia natamani wote wote bila kujali cheo chako niwatafute sehemu yenu ya kuishi halafu hii hapa nimpe Pina wangu tu ajinafasi hatakiwi kusumbuliwa kwa raha anazonipa.Lakini ndiyo siwezi, tukibaki wawili nyie mtajifunza wapi kupendana kama sio hapa.Itabidi tu mbaki na sisi hapa, mshuhudie upendo wa kweli.

Tulifika mpaka kwao, Baada ya kufika tulikuta bibi na Samwel wamekaa nje na mambo Yao wenyewe hawana habari. Samwel anampenda sana mama yake alimkimbilia kama alivyo fanya Mara ya kwanza nimefika hapa.

Nilikuwa nafurahia tu walivyo hata mama yake alisema β€œmbona husalimii.”
Mtoto huyu alinisalimia, nami niliitikia kwa upendo nikisema β€œhujambo Şam.”
Alitabasamu na kusema β€œSijambo, asante kwa kumrudisha mama yangu.”
Nilitabasamu na kusema β€œlazΔ±ma nimrudishe salama kwasababu mimi pia ni mama yangu.”

Sam alishangaa na macho yake kubadilika akisema β€œmama yako?, hapana huyu ni mama yangu mwenyewe.”
Nilicheka na kusema β€œni mama yangu pia.”
Akaniuliza kWa upole β€œkwahiyo mimi ni kaka yangu wewe?”

Nilitabasamu na kusema β€œni kweli kabisa.”
Nilimtazama Pina, alikuwa na furaha sana. Tulisogea mpaka kwa bibi, bibi alinikaribisha kwa furaha sana. Nilimsalimia kwa heshima na Şam alimsimulia bibi kuwa mimi ni kaka yake, tukacheka. Pina alisema β€œBibi anaitwa Rodricky, ndiye niliyekuwa nakuelezea kuhusu yeye.”

Bibi alitabasamu na kusema β€œkaribu sana mjukuu wangu.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

CHAGUO LA MOYO FULL

KIAPO CHA MASIKINI FULL

SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? FULL