LOML | Love Of My Life (217)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:217
Kuna muda hata niliwaza kuhusu alivyo zungumza mama yake, lakini mbona nilijitahidi mpaka mnasihi nilimtafutia, Ina maana amekuwa sex addict namna hii.

Badala ya kumchukia unajikuta unamuonea huruma uzuri ni kuwa Hana nafasi tena kwenye maisha yangu. Siwezi kuwa naye Tena siwezi kuvumilia maumivu haya.

Nikiwa nawaza hayo, simu yangu iliita, nilitazama alikuwa ni Willy. Nilipokea na kujikuta nacheka sana maana Willy alianza na kusema “baba Pina, inakuwaje unatoka husemi. Au sasa ndiyo kıla kitu Pina mimi tena hunikumbuki.”

Nikacheka na kusema “nisamehe sana kaka, nimeruhusiwa leo. Hapa nipo barabarani.”
Akaniuliza kWa upole “umepona au ni vipi?”

Nikamwambia kwa upole “nipo vizuri kaka, bado kidogo sana Ila nilikuwa namrudisha Pina.”
Akacheka akisema “ulikuwa naye, kaka wewe una balaa.”

Nilicheka nikisema “naanzaje kumuacha sasa. She is everything, she is everything I need. Wallah nakuambia hapa sina tatizo lolote. Sio malalamiko tu utasikia raha sana.”

Tulicheka tu, Willy aliniambia “nipo kwako hapa nakusubiri. Fanya haraka başı nikujulie hali niondoke zangu.”
Nilitabasamu na kusema “nashukuru kwa upendo kaka, wewe ni ndugu yangu wa faida.”

Akatabasamu na kusema “fanya uwahi baba Pina.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata