
LOML | Love Of My Life (220)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:220
Giana alisema “nashukuru sana Shem, nitazingatia hilo, uwe na siku nzuri.”
Nilitabasamu na kusema “nashukuru.”
Wakati naondoka tu, huyu mume wa Giana alinikimbilia na kusema “nisamehe sana kaka, nisamehe sana, najua utakuwa Umeona ndiyo maana umezima hata hivyo nashukuru kwa kuizima.”
Nilimtazama na kusema “Unakosea sana, unazingua sana. Najua unafahamu kama unawakosea wote wawili. Tengeneza ndoa yako, muogope Mungu na zingatia zaidi maisha yako. Uwe na siku nzuri kaka.”
Taratibu nilianza kuondoka huku huyu jamaa alinitazama tu. Nilipofika nje, niliingia ndani ya gari na dereva alishika njia kuelekea nyumbani.
Nipo njiani nakumbuka maisha ya Giana na mume wake, namna wanaigiziana maisha hata nasema “Mungu hızı sio ndoa umetaka tuwe nazo. Najua kampeni ni kubwa sana hii ya kuharibu familia.
Usituache tuangamie Mungu wetu. Ni huruma na maafa sana dunia bila familia. Ingilia kati Mungu na ütüpe mwanzo mpya.
Nafsi yangu inauma sana kuona usaliti wa namna hii ukiendelea kwenye familia zetu. Tuhurumie Mungu, na utukumbushe kuwa ndoa zinatoka kwako wewe mwenyewe na wewe ndiyo mlinzi wetu.”
Nikiwa nakaribia nyumbani, ujumbe uliingia kwa simu yangu nilivuta simu haraka. Nilipotazama alikuwa ni LOML❣️, Nilitabasamu na kusoma, Aliandika “Nakupnda(nakupenda) sn(sana)Ricky, thanks 4loving(for loving) me, I miss you My Fate.”
Nilitabasamu, nilitamani Kama na mimi nimuandikie ujumbe Ila hawezi kusoma. Niliamua kumpigia tu. Haraka alipokea akisema “I was dying waiting for this call.”

