
LOML | Love Of My Life (222)

๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ:222
Nilijikuta nacheka na kukata simu nikisema โhana akili huyu mtoto.โ
Willy akasema โsijawahi kukuona na furaha namna hii. Sasa haya ndiyo mapenzi, mapenzi yenye tu vitu vitu bila kujali umri unacheka kama jinga.โ
Nilicheka nikisema โna ataniua kwa raha. Sijawahi jihisi hivi maisha yangu yote.โ
Tulicheka.
Nilimuomba mama Babuu atuandalie chakula kilekile nilichokula wakati nikiwa na Pina. Na Willy tulikula pale kwa furaha akisifia chakula kizuri. Eenh basi ikawa raha muda wote unatamani umsifie mpenzi wako.
Zamanฤฑ nilikuwa namshangaa mtu kฤฑla kitu my baby, my love, kafanya hivi kafanya kile. Nilikuwa naona washamba, kumbe mimi nilikuwa sijui kupenda.
Vinawasha kฤฑla muda unatamani umsimulie mtu, kฤฑla muda unatamani watu wajue una mpenzi mzuri, kฤฑla muda unatamani mambo yawe ya raha tu. Ndiyo yamenikuta sasa. Kama wewe humtaji mpenzi wako, usiwaonee wivu wanaosifia wa kwao. Mapenzi yanawasha useme tu muda wote. Ni raha.
Tuliongea Mengi na rafiki yangu lakini zaidi kuhusu taraka ingawa mpaka muda huu sikuwa nimemwambia nini shida. Kwasababu sikuwa naweza kusema kabisa naona aibu sana. Baลฤฑ nilimpigia mwanasheria. Alikuwa ni mwanamke nakumbuka sana.
Baada ya kumpigia aliniambia โkesi yako imeisha ni rahisi sana. Hapa ni kupata tu na urahisi kanisani ugumu Labda aweke huyo mwanamke lakini kwakuwa anajua kosa lake baลฤฑ hana cha kufanya maana haikubaliki kabisa. Wewe ukipata nafasi tukutane tuanze kufuatilia hili ni ndani ya muda mfupi limeisha na baba yako amesisitiza iwe haraka sana.โ

