LOML | Love Of My Life (223)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:223
Nilitabasamu na kusema β€œnashukuru sana, kesho nitawahi kanisani Kisha nitakupa mrejesho.”

Mwanasheria alinipa baraka zote na Kisha nikaendelea na mambo yangu. Muda ulifika Willy aliniaga kwa upendo na akinitaka nipone haraka turudi kazini nami nilimwambia kuwa kesho nitakuwa ofisini Kwahiyo hakuna muda wa kulala. Nilifurahi sana.

Najua mtasema nawanyanyasa eenh, Ila acha niseme tu usiku huu tena niliwasiliana na LOML na Baada ya hapa nilikunywa dawa na kupumzika. Siku iliyofuata niliamkia kwa Padri kuzungumza naye juu ya jambo hili.

Aliponiona ofisini kwake alisikitika tu kwasababu ni mtu ana heshimiana sana na baba yangu. Sikuwa na neno zaidi ya kumsalimia na aliniambia β€œkaribu sana kijana wangu. Leo sina furaha kabisa kwasababu ndoa yako tangu niwe padri na nifungishe ndoa.

Yako ndiyo ndoa ambayo haijadumu hata kidogo. Miezi 6 tu, roho yangu inaniuma sana, roho inaniuma kupita kiasi. Lakini nataka nikuulize kuwa haya niliyosikia ni kweli, kama ni kweli nataka kusikia kutoka kwako.”

Nilimtazama tu Padri na Kisha nilianza kumuelezea. Alisikitika sana, alisikitika hata alitaka kulia akisema β€œroho inaniuma siwezi shauri ndoa hii. Kijana wangu pole na yote, tulijitahidi awali kwa sasa başı Sina namna naungana na wewe. Ukihitaji msaada wangu wowote ule nipo tayari. Vipi ushafungua shauri La taraka.”

Nilimuona anavyoumia, nilimtazama na kusema β€œkila kitu tayari kwa mwanasheria.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

SIMULIZI YA INGIZA FULL

SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? FULL

BINTI MDUNGUAJI FULL

TOBO LA PANYA FULL