LOML | Love Of My Life (225)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:225
Nilimtazama na kusema β€œamekuambia ndivyo mama. Nilimfukuza na kusema kweli sitaki kumuona. Ni kweli nina mahusiano na Pina, anaitwa Pina mama. Sio kipofu hiyo ni changamoto tu na inaweza kukuta au nikuta ni jambo la kawaida.

Kusema kweli mama, sitaki kumzungumzia hapa Gabby. Ila tayari nishaanza fuatilia taraka. Simtambui tena na haraka sana nitampa taraka na kama kuoa ni Pina na Sio Gabby.”

Mama alinitazama na kusema β€œsio kweli mwanangu, Haiwezekani kabisa wewe kumuoa huyo Kipofu. Nitaelewa humtaki Gabby kwasasa walau tafuta wa kuendana na sisi.

Sio yule, na Gabby kwani ana kasoro gani binti wa watu mzuri ana sifa zote kwani una shida gani kijana.”

Simu yangu iliita, ilikuwa natakiwa kutoka, nikamwambia mama β€œkama unavyo ona sijakuwepo kazini muda mrefu. Nina kazi nyingi. Mama unaonaje tukipata muda tuongee kuhusu ndoa yangu na Pina sio na Gabby tena.”

Mama alinikata jicho, nikacheka na kusema β€œnakupenda mama Ricky, baadaye basi msalimie baba mwambie nampenda sana.”

Mama alisema β€œtena huyo mama yako ndiyo anakuponza kabisa siwaelewi.”
Mimi nikacheka tu.

Mida ya saa tatu hivi ndiyo nilimaliza. Unajua hata nashangaa nimeachana na Gabby naona kazini kuna changamka, kazi ni nyingi balaa, unapata kazi kampuni mbali mbali mpaka namshangaa Mungu. Kuna watu ukiwa nao kwenye mahusiano hata maendeleo ya kazi ni magumu sana. Sasa hivi naona mambo ni mazuri sana kwangu hata mauzo nimekuta yamepanda sana ofisini na namshukuru Mungu kimoyomoyo huku nikiwa najisemea sadaka ipande hapa.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

LOML | Love Of My Life FULL

SHEM MI NATAKA FULL

KIAPO CHA MASIKINI FULL