
LOML | Love Of My Life (226)

ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:226
Nilimpigia Pina na kusema βLoml, mimi ndiyo napata muda sasa. Naweza kukuona kweli?β
Pina alisema βhaki ya Mungu Ricky walau nikuone hata kidogo tu nimekukumbuka sana.Nitashindwa kulala, nakumiss eti.β
Nikatabasamu tu na kusema βnakuja.β
Basi nilipita supermarket. Nilinunua vingi kwaajili ya mahitaji ya nyumbani. Nikaweka kwa gari na safari ilianza. Nilipofika nikampigia simu, alitoka nami nikampokea kwa furaha akaingia ndani ya gari. Alinikumbatia akisema βI missed you so very much.β
Nilitabasamu na kusema βmimi zaidi mpenzi.Lakini naomba vumilia, kuna mambo nafuatilia na kazini sasa mambo yamekuwa mengi sana. Nakukumbuka muda wote lakini nakuwa sina namna. Niombee suala la taraka liende vizuri na kazini nako mambo yazidi kuwa mazuri.β
Alitabasamu na kusema βamen mpenzi, asante kwa kuja kuniona.β
Nilimbusu na kusema βnimekuwa na siku ngumu sana. Naomba niende sasa ila kuna mzigo wako hapa.β
Basi alitabasamu tu nilimshushia vitu na kusaidia kubeba. Akawa ananishangaa tu, kisha nilimpa pesa mkononi na kumbusu nikisema βtutawasiliana mpenzi wangu nakupenda.β
Aliniambia kwa upole βRicky Nakupenda.β
Nilitabasamu tu.
Kabla sijafika hata nyumbani alinitumia ujumbe βthanks for taking care of me and my family.β
Nilitabasamu tu, anaweza walau kuniandikia ujumbe japo sijui namna gani anateseka. Ingawa najua kuna watu wenye macho simu za button hata akifumba macho hakosei. Nilimpigia akawa hata anataka kulia basi tunacheka hata nilifika nyumbani.

