
LOML | Love Of My Life (227)

ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:227
Sijui nikuelezee vipi, maisha yangu na Pina yalikuwa mazuri sana. Alikuwa ni mpenzi wa kuniombea asubuhi kila ninapotoka. Alikuwa ni mpenzi wa kunitia moyo na kunipa furaha. Alikuwa ni kila kitu nahitaji. Baraka na milango yangu kazini ni mvua ya baraka na mfanikio. Kila kitu kilikuwa sawa kabisa. Mambo yalikuwa mazuri. Nilikuwa napata kazi nyingi mpaka nasahau kula. Unajua sasa kilichokuwa kinatokea, Pina ana wasiliana na mimi ananiagizia chakula kwa boda. Nafurahia sana maisha haya.
Baada ya siku tatu mwanasheria wangu alinitafuta. Kila kitu kilikuwa tayari. Kusema ukweli nilifurahi sana. Na nilienda mpaka nyumbani kwao Gabby. Nilipofika pale niliwaelezea shida yangu kwa Gabby. Nakumbuka Gabby aliitwa na nilimkabidhi.
Gabby alinitazama na kuanza kulia, alilia akisema βbaba naomba nisaidie, mama nisaidieni tafadhali mimi maisha yangu bila Ricky bora kufa. Naomba nisaidieni siwezi kuachana na Ricky kabisa. Nipo tayari kufanya lolote ila sio kumuacha. Siwezi baba.β
Nilimtazama tu vile analia, niliaga nikisema βmimi naondoka, Gabby jumatatu tunatakiwa kuonana maelekezo yote yapo hapo.β
Aliita kwa huruma βRicky tafadhali!!β
Mwanaume najali sasa, niliondoka kwa mgandisho kabisa kwa kujiamini, hapa ndiyo na mdundo wa kishujaa una sikika. Nimeweza na sijamuhurumia tena. Niliingia kwa gari na kurudi nyumbani. Kusema kweli sikuwa namshikirisha kabisa Pina haya mambo yangu na mke wangu, nilitaka nipate taraka niwe huru naye kabisa. Sikutaka kabisa kumuhisisha na haya mambo.
Hivyo kesho yake asubuhi baba yangu alinipigia. Nilipokea na aliniambia βkijana wangu, njoo nyumbani.β
Nilishangaa na kuuliza βkuna tatizo baba?β
Baba alisema βkuwa jasiri sana, hakikisha unafanya maamuzi sahihi kuna wageni wako hapa.β

