LOML | Love Of My Life (228)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:228
Nilivuta pumzi na kusema β€œnakuja baba.”
Nilijua tu, ni Gabby na familia yake. Nilijiandaa na kuanza safari yangu. Nilifika na kweli nilikuwa sahihi kabisa. Nilikuwa mimi na wazazi wangu na Gabby na wazazi wake. Alivyo ni kama amekesha analia.

Baba yake alianza kwa kusema β€œpole kwa kukusumbua asubuhi kijana wangu. Najua umefanya maamuzi lakini sisi kama wazazi tunatamani kuwasaidia. Tafadhali mnaweza kuwa wawazi walau tupate wapi tunaanzia.”

Mama yangu alisema β€œkabisa, baba yenu yupo sahihi. Binafsi nipo njia panda na natamani kusaidia hii ndoa isife. Eti Binti yangu nini kimetokea?”

Gabby analia, mama yake ana mbembeleza sana. Analia akisema β€œnimekosa jamani, nilimkosea mume wangu naahidi nimekosa kabisa sijui hata nina shida gani, nahitaji msaada mimi nisaidieni lakini sio kumkosa Ricky. Yeye ni maisha yangu.”

Nilimtazama na kusema kwa upole nikiwa na uchungu mbele ya familia β€œGabby unaweza ukaacha maigizo hapa. Wazee wangu, ninyi ni wazazi wangu na sina sababu ya kuwaficha. Mimi na Gabby ndoa yetu haiwezi kuwa.

Amenifanyia mengi mabaya, awali niliwasikiliza na nilikuwa tayari kusimamia ndoa yangu. Najua amewaambia namsaliti na wakati anajua fika sijawahi hata mara moja zaidi ya kumpenda yeye.

Amenifanyia mengi mabaya sana na kusababisha matobo kwenye moyo wangu. Sitaki kumuona wala kumsikia na sio mimi tu.

Hafai kuwa mtu yeyote kwasababu mbali na yote, Gabby nilimshuhudia mimi kwa macho yangu, ndani kwangu, kutandani kwangu akifanya mapenzi na mwanamke mwenzie, alikuwa na Giana, Mke wangu ni msagaji, hafai, simtaki, simtaki.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata