LOML | Love Of My Life (229)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:229
Ule uchungu ukazaa machozi, nikasikia mama yangu akisema huku mikono kaweka kichwanu na mara ashikr kifua chake β€œyereweiiiiiiiiiii, Bikira maria mama Wa Yesu, Yeeemweeeee tataaaaaaaaaa!!, uwiiiiiii uwiiiii uwiiiii we mtoto, mwili wote unatetemeka mimi.”

Mama yake palepale alianguka, baba mtu alikuwa ameduwaa mimi na baba ndiyo kutoa msaada kwa huyu mama Gabby wakati huo Gabby ametoka nje mbio analia. Mama yangu hajui ashike nini aache nini.

Tulimchukua huyu mama na kumfanyia utaratibu aende hospitali. Baba na baba Gabby ndiyo walitangulia, mama aliniambia β€œkwanini hukuniambia, kumbe mtoto shetani huyu.”

Nilimtazama mama na kusema β€œwewe ni mama yangu. Unajali furaha na pesa muda wote. Hujui nyakati zangu za huzuni nataka nini, huwezi kunitetea wala kunishauri.

Ulisimama upande wake kuliko kunihoji mimi nateseka na nini. Tangu awali nilikuwa sipo tayari na ndoa hii ila ulisimama kidete kwasababu tu ni mtoto wa kitajiri.Huyo ndiyo Gabby mama, mimi nawahi kazini. Tutawasiliana.”
Mama alibaki anashangaa tu machozi yakimtoka.

Nilijisikia nafuu sana, niliendesha gari nikiwa natokwa na machozi ya furaha. Nilikuwa nawaonea huruma sana wazazi wake kujua jambo kama hili. Halikuwa jambo zuri kabisa ila ilikuwa ni lazima iwe hivi. Kusema kweli siku hii pamoja na uzuri wake sikuwa na raha sikuweza hata kufanya kazi nikarudi nyumbani mapema kabisa ingawa tulikuwa na kazi nyingi sana.

Ilikuwa jumamosi, jumapili ilikuwa niende kanisani sikwenda sikuwa sawa. Nilikuwa najiona kama nimetoka sijui kwenye shimo gani na nipo huru. Nilikuwa na furaha ambayo imepitiliza imekuwa kama huzuni na kumbe ni furaha. Nakumbuka niliwasiliana na Pina. Uzuri ni muelewa sana yeye ni kunitia moyo tu.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

BIOLOGY TEACHER FULL

LOML | Love Of My Life FULL

SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? FULL