LOML | Love Of My Life (230)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:230
Nakumbuka sana siku hii ilikuwa jumatatu, ilikuwa niende kufuatilia mambo yangu ya taraka. Nilipofika pale mwanasheria alikuwa ana furaha tu akisema β€œkila kitu kimeisha. Binti amekubali kirahisi sana. Ingawa alikuwa analia lakini baba yake amefanya mambo kuwa rahisi mno.”

Nilishangaa nikiuliza β€œunataka kuniambia imekwisha.”
Alitabasamu na kusema β€œimekuwa zaidi ya tulivyo tarajia hongera sana.”

Nlifurahi ingawa najua kwa baba na mama Gabby ni maumivu. Nilichukua bahasha yangu na moja kwa moja mpaka hospitali. Nilipofika nilimuona baba Gabby amejiinamia. Nilienda mpaka alipokaa, nilimgusa Bega. Aliinua uso wake na kusema β€œkijana wangu.”

Aliinuka na kunikumbatia, baba alilia sana huyu. Nikamuuliza β€œmama anaendeleaje?”
Alishusha pumzi na kusema β€œMungu ni mwema.”
Nilitabasamu na kusema β€œasante sana baba.”

Alinitazama akilia na kusema β€œwewe ni kijana mzuri sana. Hata mimi nisingeendelea na mwanamke aliyevuka mipaka namna hii mwanangu. Unatakiwa kuishi maisha mazuri. Gabby ni binti yangu naumia amepoteza kijana mzuri kama wewe na kujiingiza kwa laana kama hii. Nini kinaikumba familia yangu.

Tusamehe sana, tusamehe sana mwanangu.Naomba undugu wetu usife wewe ni kama mwanangu.
Nilimkumbatia huyu baba kwa uchungu, na wakati huo simu yangu iliita. Nilitoa mfukoni pale juu inasomeka β€œLOML❣️”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

SHEM MI NATAKA FULL

JOGGING MASTER FULL

NILIMPENDA KUPITA KIASI FULL