LOML | Love Of My Life (231)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:231
Baba alinitazama akatabasamu na kusema “nenda, nenda katafute furaha yako.”
Nilijikuta nacheka, nikapokea ile simu nikiwa na furaha nikisema “jiandae nakuja sasa hivi nakuja.”
Pina alisema kwa upole “una nini?”
Nilicheka nikisema “yamekwishaaaaaaa, yamekwishaaa.”


Nilikata simu, nikampigia baba, nikampigia Willy. Nilikuwa na furaha sana siku hii.
Nilifika mpaka Nigeria kwao Pina. Sio Nigeria nchi, ni hapahapa bongo. Nilikuta bibi akiwa ana kazi zake. Nilimsalimia kwa furaha.

Pina alitoka akiwa amependeza ingawa alikuwa na nywele zake za mia tano. Nilitabasamu kumuona na kusema “bibi naweza kumuiba huyu mrembo mpaka hapo kesho au kesho kutwa hivi au mtondo.”

Bibi alicheka akisema “nitakufunga Rodiriki.”
Nilicheka na kumkumbatia nikisema “umependeza sana cha madeko wangu.”
Alitabasamu akisema “una furaha sana.”

Nilicheka nikisema kwa sauti ya chini “yamekwisha, sio mume wa mtu tena.”
Pina alifurahi akanikumbatia tukirukaruka, hata bibi akawa anashangaa akisema “naomba muende mnachanganyikiwa.”

Tulicheka, bibi akasema “Mungu atunze furaha yenu.”
Niliitikia “Amina bibi Rodiriki.”
Tulicheka sana. Fimbo nikaacha pale nikisema “utakuwa na mimi, mimi fimbo yako mimi macho yako.”

Bibi anacheka tu. Nilimbeba jui juu mpaka kwa gari akicheka sana. Basi kwenye gari mziki sana, nilikuwa na furaha. Nilimpitisha sehemu za nguo nzuri akabadilisha akabeba na zingine na za kulalia eneh najisikia tu kutumia hela kwaajili yake na mtoto wake hata bibi yake. Sikuwa naumia kabisa nafanya kwa mapenzi kabisa.

Nilimpeleka kwa wauza wigs kali sana wakamtengeneza. Huyu mwanamke sio wa kawaida ni mzuri sana. Tulipita mahali tulikula, sikuwa nataka kuongea kitu nataka tu kufurahi.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata