
LOML | Love Of My Life (236)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:236
Nilicheka na kusema “Niache nakuambia hapa nilipo mwili hauna nguvu hata moja. Tukale emu.”
Tukacheka.
Nakumbuka tulijiandaa vizuri, nikamchana na wigi lake. Akavaa Tena nguo nyingine nzuri. Mimi natabasamu tu nikimuona. Nilimshika mkono na kusema “Unajua wewe ni mzuri sana Pina. Natamani ungejiona ulivyo.”
Akatabasamu na kusema “piga picha ili unitunzie ipo siku nitaona si hata wewe una amini hivyo?”
Nilitabasamu na kusema “nitahakikisha hilo linatokea. Utaona tena baby.”
Alitabasamu na kusema “kiti Pekee natamani ni kukuona wewe mpenzi wangu. Natamani sana.”
Nilitabasamu na kusema “itakuaje Kama utafungua macho yako na usinipende.”
Alitabasamu na kusema “nimechanganyikiwa, napenda sana moyo wako, kilicho baki ni kuona tu mmiliki wa moyo huu wa kipekee. Mimi nakupenda vyovyote utakavyokuwa. Unaishi hapa moyoni mwangu.”
Nilitabasamu na kusema “Nakupenda.”
Alitabasamu na kusema “Nakupenda.”
Başı taratibu tulitoka, tulitoka mpaka dinning. Vile tumetoka mama Babuu alitupokea kwa upendo sana akitabasamu na kusema “mnapendeza sana. Eenh wanangu mmeamkaje?”
Tulitazamana na Kisha nilisema “tunashukuru Mungu tumeamka salama.”
Alitabasamu na kusema “karibuni sana, hata mimi nawaona mpo vizuri kabisa.”
Tulicheka.
Taratibu niliandaa kiti ya Pina, nilihakikisha amekaa vizuri. Na Kisha Baada ya hapo sasa na mimi nilikaa karibu yake, nikamuwekea kıla kitu sawa kutokana na hali yake.
Tulisali na Baada ya hapo sasa nilianza kula na kumlisha. Alikuwa anatabasamu akisema “Asante sana mpenzi, nashukuru.”
Nilitabasamu na kusema “nilikuambia kıla kitu kwaajili yako. Mpenzi nina furaha sana. Sijui hata nikuambie kitu gani, lakini wewe amini Nina furaha sana na nipo huru sasa. Hivi utapakumbuka hapa.”
Alitabasamu na kusema “hujui tu furaha ya moyo wangu Mpenzi wangu. Nina furahia kıla kitu. Nashukuru sana mpenzi wangu.”
Nilitabasamu, nikatoa simu nikapiga picha ya pamoja na yeye aliuliza “mbona kimya huongei?”
Nikasema nikitabasamu “weka pozi napiga picha mimi.”
Başı tulikuwa na furaha hata nikawa namwambia mazingira naishi na mtaa vitu Kama hivyo.
Tukiwa na hali hiyo, mlangoni palibishwa hodi. Mama Babuu alienda kufungua. Nikawa namsikia akisema “karibuni sana, karibuni.”
Mimi nikajiuliza “nani tena hawa mida hii.”
Vile wanaingia ni mama na baba yangu. Nilitabasamu kuwaona na kusema “mama karibuni sana, baba karibuni.”
Baba alifurahi sana, alifurahi hata alimfuata Pina na kusema “mwanangu umependeza sana. Umebadilika sana. Mzuri sana mwanangu.”
Pina alitabasamu na kusalimia kwa heshima sana “shikamoo baba, karibu sana.”
Baba aliitikia kwa furaha, mama yangu sasa alivyokuwa anamtazama, nilimtazama na kumpa ishara amsalimie. Lakini mama hakufanya hivyo, Pina alisema tu “mama shikamoo!!”
Mama alichukua muda kujibu na Kisha alijibu hata nilitazamana na baba yangu. Lakini Pina wala hata hakujali. Alinitazama na kusema “mpenzi nipeleke chumbani.”
Nilitabasamu kivivu maana mama alikuwa amenitoa kwenye furaha yangu. Kisha taratibu tulifika chumbani. Nilimshika Pina na kusema “baby please usijali kuhusu mama yangu.”
Alitabasamu na kusema “najua hapendi uwe na mimi. Lakini wala hata sijali kwasababu baba ananipenda na wewe unanipenda sana. Başı nasubiri kama na yeye itatokea atanipenda.”
Nilitabasamu na kusema “nafurahi unatambua hilo. Ninayo imani atakufahamu na mtaelewana vizuri sana. Ni masuala ya muda tu.”
Alitabasamu, lakini unajua mtu akijisikia vibaya eenh macho yake yanazungumza zaidi. Nilijisikia vibaya Ila nitafanya nini sasa ndiyo imeisha kuwa hivyo naumia moyoni Ila sina La kufanya.
Nakumbuka nilijikuta napoteza tu furaha. Başı nilitoka taratibu sana, nikasikia baba yangu ana mwambia mama yangu “mke wangu hivi ni kitu gani haswa kinafanya unamchukia hivyo Yule binti. Amekukosea wapi, umewahi kukutana naye kabla, au anaharibu nini kwenye maisha yako eenh!!”
Mama alinyamaza tu na baba aliendelea “unatia aibu sana, maisha gani hayo eenh. Tungekuwa tunaangalia madhaifu unafikiri tungekuwa wapi leo maisha haya.
Badala umfurahie mtoto, umpongeze katoka kwenye shimo La laana wewe tena unaleta mambo yako Kwahiyo unataka awe na yeye na mwanaume mwenzake wa kukoboa naye au unataka nini?”
Mama alisema “baba Ricky ni maneno gani tena hayo. Mimi Sina maana hiyo kabisa.”
Baba alisema “nini sasa mtoto wa watu mzuri kabisa hana shida yoyote hutaki unataka wakina Gabby.”
Mama alinyamaza na mimi ndiyo nilitoka. Baba aliponiona tu aliniuliza “kijana wangu upo sawa?”
Nilisema kWa upole “nipo sawa baba karibuni sana.”
Baba alisema “tusamehe sana mwanangu, tumekuja bila taarifa lakini binafsi nilikuwa na furaha sana Baada ya mwanasheria kunipa habari. Kusema kweli mwanangu Mungu amekuepusha na balaa kubwa sana. Mimi kama baba yako nina furaha sana.”
Nilishusha pumzi na kusema “baba wewe ni mtu bora kuwahi kutokea kwenye maisha yangu. Upo na mimi hatua kwa hatua. Nashukuru sana na naona kıla kitu. Baba nashukuru sana na unajua ninavyo kupenda sana. Nakupenda sana baba yangu.”

