
LOML | Love Of My Life (238)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:238
Machozi yalimtoka, alilia hata nikaogopa. Nilimsogelea na kumuuliza “Pina shida nini?”
Aliniambia kWa kulia, “naogopa sana mimi, ninaogopa mno Ricky. Hivi unaona ni kawaida eenh, kıla mama mkwe hanipendi mimi. Nina shida gani. Naona kama hii Hadithi Ina nirudia Tena kwa namna ya pekee sana. Sijui hata nifanye nini Ila naogopa kila kitu.”
Nilimtazama na kusema kwa upole “Unataka kuniacha mwenyewe mpenzi?, inajirudia vipi najua huoni, ina maana hata kuhisi huu upendo huwezi?, sawa tufanye kuhisi umeshindwa hata sauti yangu husikii, sauti ya baba yangu pia husikii kipenzi. Kwanini unafanya hivyo?”
Alinitazama tu, nilimwambia na kumfuta machozi nikisema “sitaweza kukubali nikishuhudia wewe unalia Pina. Wewe ni mwanamke ninaye kupenda kuliko kitu chochote Naomba wala usilie. Tumuombe Mungu mambo yaende Kama ambavyo sisi tunataka.
Tuishi sasa na tuanze kujaza nafasi kwenye Yale mashimo ambayo tumesababishiwa zamani. Nakupenda Pina Madeko wangu, Nakupenda LOML, Nakupenda.”
Alilia kWa furaha na kunikumbatia na aliniambia “Asante kwa kunifanya wako.Unanitoa wasiwasi na kunipa sababu ya kupumua kıla wakati. Ninakupenda sana, ninakupenda.”
Nilitabasamu na kusema “haya sasa tujiandae uende nyumbani baby wako nikatege hela za kukupa ili usiteseke.”
Pina alicheka na kusema “sio kutafuta?”
Nilicheka na kusema “hela inategwa ukitafuta unaishia kuwa maskini mbona tega pesa.”
Alicheka kidogo ingawa naona kabisa hana furaha ile ya awali Ila nitafanya nini lazıma nimchangamshe.
Nilimsaidia na Pina wangu kuwa sawa. Niliandaa na mifuko vizuri huku nikimwambia kwa upole “Mpenzi wangu hızı nguo nataka zivaliwe, sio unaenda kupamba ndani. Nataka zivaliwe na upendeze muda wote hata kama huendi popote pake sijui unanielewa.”
Alitabasamu na kusema “nakuelewa vizuri sana.”
Nilitabasamu na tulianza kutoka mimi nikiwa nimemshika kwa upendo sana. Nakumbuka tuliposhuka mama Babuu alitufuata na kusema “Boss kuna maagizo yoyote?”
Nilitabasamu na kusema “Hakuna mama Babuuu ubaki salama.”
Mama Babuu alimtazama Pina kwa upendo, sijui alikuwa anasikia mazungumzo ya mama. Lakini alisema “Pina mwanangu, karibu sana. Kusema kweli nimekuzoea sana. Utarudi lini?”
Pina alitabasamu na Kisha alinigeukia ni Kama alitaka niseme jambo. Nilitabasamu na kusema “jibu swali Pina mimi sihusiki lakini hata mama nilikuwa nikuulize maana nimekuzoea.”
Tulicheka tu, Kisha Pina alisogea kwa mama Babuu, alianza kumpapasa mikono usoni, na Kisha alimshika mikono yake yote na kusema “Asante sana mama Babuuu. Hata mimi nimekuzoea. Nawashukuru sana kwa Upendo wenu. Nitarudi hapa tena na tena na tena na tena, si ndiyo mpenzi nakaribishwa.”
Nilitabasamu na kusema “hapa ni kwako mama, muda wowote mama Babuuu huyo hapo.”
Tulicheka na mama Babuu akasema “Ukihitaji kitu niambie tu hakuna shida.”
Alitabasamu na kusema “namba yako, namba yako ni muhimu nikitaka kuja kama hayupo.”
Tulicheka tu.

