
LOML | Love Of My Life (239)

๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ: 239
Niliwaacha wafurahie na Kisha Baada ya hapo walikumbatiana tena na tuliondoka mimi nikiwa ndiyo macho yake.Tuliingia ndani ya gari na safari ilianza.
Nilikuwa najitahidi kumfanya atabasamu lakini namuona kabisa hana furaha ilinibidi tu nimuongeleshe nikisema โPina wangu, Pina madeko wangu.โ
Alinitazama na kuitika โnaam kipenzi.โ
Nilimwambia kWa upole nikisimamisha gari โNashukuru sana kwa penzi lako tamu nashindwa hata kuelezea. Usiku wa Jana ulikuwa usiku wa kihitostoria kwangu. Wewe ni mwanamke wa ajabu, ni mwanamke wa pekee.
Umenifanya nifurahie sana mapenzi yangu, umenifanya nijihisi wa pekee sana kipenzi. Nakupenda, nakupenda kuliko kitu chochote. Umefanya nikupende zaidi, umefanya nione namna mapenzi yalivyo ni ya muhimu kuliko kitu chochote kile.
Mpenzi sitaki, siwezi wala sipo tayari kukupoteza wewe. Na hapa nataka kukuelezea kuwa nakuomba sana, niombeee, niombee sana ili nitimize kwako majukumu kama mwanaume, nikutunze na kukulea kwa upendo sana.
Ninakupenda, Ninakupenda na viungo vyangu vyote. Usimpe shetani ushindi mpenzi. Mungu ameruhusu hili, huoni kฤฑla kiti ni Mungu. Tupo pamoja kwasababu Mungu ametaka. Niamini ninaposema Nakupenda.โ
Pina alitabasamu na kusema โni tofauti kabisa Ricky, nikiwa na wewe siogopi kitu. Najiona salama kabisa. Mimi hapa nilipo sitamani kukukosa, sitamani kukupoteza.
Natamani niwe ngozi yako ili nikugande ulipo nipo na nilipo upo. Mpenzi nakupenda sana. Nakushukuru kwa huu upendo wako, ni mkubwa sana.
Nawaza unawezaje kuwa na roho nzuri namna hii. Kwa mtoto wangu, kwa mama yangu nakosa majibu kabisa. Wewe ni bingwa, wewe ni Bora na wa thamani sana. Nakupenda.
Ndiyo maana nasema wewe ni hatima yangu, wewe ni bahati yangu. Ninakupenda na nakuahidi kuanzia sasa hivi sitakubali tena maisha yangu ya zamanฤฑ yanitafune. Unanipenda sana, nakupenda sana.โ
Tulikumbatiana kwa upendo sana. Kisha niliwasha garฤฑ mpaka nyumbani kwao. Baada ya kufika nilimshusha na kushusha vifurusi vyake. Na bibi yake tu ndiyo alikuwepo. Nilimuuliza โSam kaenda wapi?โ
Alitabasamu na kusema โshule.โ
Nilimtazama na kusema โmimi nawahi kazini, tutawasiliana na si unajua ninavyokuwa natingwa eenh.โ
Alitabasamu na kuniambia โhukai hata kidogo.โ
Nilisema kWa upole โUmeanza hivyo, tulia hapa na bibi. Bibi Naomba nichungie.โ
Bibi alicheka, na Kisha alinishika mikono yangu na kusema โmjukuu wangu, Nakushukuru sana kwa chakula. Mungu azidishe baraka kwenye hii mikono iliyotoa kwaaajili yetu. ฤฐle sehemu umetoa ikazae Mara nyingi sana na kurudi Mara dufu.
Mjukuu wangu uwe kichwa na sio mkia. Uwe na mafanikio makubwa sana zaidi ya sasa. Uwe kijana wa faida na wala sio hasara. Nashukuru sana.โ
Nilitabasamu na kusema โNinapokea baraka zako Bibi.Amen.โ
Bibi alifurahi sana.
Na mimi nilikumbatiana na wao wote, unajua tena uswahilini macho yapo Ila najali sasa sijali lolote.Nilikuwa na furaha tu.Niliagana nao nikimwambia Pina โnipigie, au nitakupigia muda wowote sawa mpenzi.โ

