LOML | Love Of My Life (240)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️: 240
Ananiaga tu ana tabasamu. Nilimuacha pale na bibi yake waliingia ndani na mimi nikaondoka zangu. Walikuwa na furaha na mimi nilikua na furaha sana. Hivi umewahi kaa zako tu na mambo yako, ukakumbuka ujinga wako ukiwa na baby wako unajikuta unacheka.

Başı nipo ndani ya gari nikikumbuka usiku natabasamu, Mara nicheke, Mara nisisimuke. Halafu najisemea “Pina utaniua, utaniua mama, utaniua!!”

Wakati huo simu yangu iliita alikuwa ni Nilitabasamu tu, mpaka akili yangu ina hama nikijua tu ni Pina ananipigia.

Nakumbuka nilipokea na alisema “baby umezidi sasa, zawadi zote hizi kumbe umeniwekea na pesa?”

Nilicheka kidogo na kusema “sasa mke wangu atatumia nini. Tumia pesa mama, zoea pesa ikuzoee. Unajua tangu nimekuwa na wewe napata pesa zaidi.

Hii maana yake ni nini?, maana yake ni kuwa una baraka nyingi sana sasa lazıma na wewe ule. Hata hivyo kama nyumbani chakula kimeisha unasema nataka unenepe mimi.”

Pina alicheka na kusema “unajua unazidisha sasa chakula halafu hizi pesa si ndiyo matumizi yake.”

Nilisema kWa upole “hapana mimi nafanya kazi kwanini mama, unastahili zaidi ya hayo. Tulia, tulia nikupende mama.”
Pina alicheka tu na kusema “bibi anashukuru sana kwa zawadi. Kama namuona jumapili atakavyo pendeza.”

Nilitabasamu na kusema “sana, Mwambie atapendeza jumapili zote muhimu tuwe wazima.”
Mimi nacheka tu. Başı tulicheka pale na kuagana na mimi nikaingia kazini.

Başı nimefika kazini, naingia tu ofisini nakutana na Willy anasema “kaka kazini saa 7 kaka tunafanya kazi kweli?”
Nilicheka na kusema “acha tu ndugu yangu, Acha tu.”
Willy alimalizia “Kwisha habari yako huyo ni Pina.”

Nilicheka na kwenda kukaa, ile nakaa aliniambia “imekuaje Jana ndugu yangu mbona haraka imetoka hiyo taraka.”

Nilimtazama na kusema “ndugu yangu, ndugu yangu Mungu ana manguvu sana. Nilikuwa natamani iwe hivyo na imekuwa. Kutokana na ukubwa wa tatizo, baba yake mwenyewe aliingilia kati na kutaka binti yake akubali taraka itoke.

Ndiyo ikawa hivyo. Sikuamini Kwahiyo hapa nilipo ni free man. Jana nimesherekea na Pina wangu.”
Willy alinitazama na kusema “ina maana kuniambia kilichotokea huwezi kabisa.”

Nilimtazama na kusema “kaka ukurasa wa Gabby funga. Fungua ukurasa unaofuata ukutane na simulizi nzuriiii, simulizi tamu ya mapenzi.”
Willy alicheka.

Mimi ndani ya moyo wangu nimemalizana na wazazi sioni haja ya kuendelea kuzungumza udhaifu wa Gabby nje ya hapa. Atajua yeye na Mungu wake, na maisha yake mwenyewe mimi hayanihusu tena.

Nilimwambia Willy “wewe ni kaka yangu, Asante kWa kuwa na mimi nyakati zote. Ninakushukuru na nina deni kubwa sana kwako. Sina cha kukulipa kaka Ila Mungu atusaidie tu.”

Willy alinitazama na kusema “wewe ndugu yangu bhana. Eenh niambie.”

Nilicheka na kusema “nikuambie nini ndugu yangu, niseme nini tena zaidi ya nina furaha sana, nina furaha mno. Lakini kuna tatizo.”
Willy alinitazama na kuniuliza “nini tena?”

Nilisema kwa uchungu “Tatizo ni moja tu, mama yangu, mama yangu hajamkubali kabisa Pina. Anamuonaje sijui hajatanguliza utu zaidi anafanya Pina ajisikie vibaya sana.”

Willy alinitazama na kuniuliza “unafikiri nini kuhusu hili kaka, unaona litakuwa endelevu?”

Nilimtazama na kusema “sijui kaka, naona mapicha picha na sitaki mtoto wa watu alıe kwasababu yangu. Hapa nataka nikimaliza mambo yangu nipate muda wa kuzungumza na mama yangu.”

Willy aliniambia “wazo zuri ndugu yangu, na vipi kuhusu Yale macho siku ile ulisema wameenda kWa dr.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata