LOML | Love Of My Life (242)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️: 242
Hata hili sikuwa naona kabisa kama naliacha.Ndani yangu nilikuwa naona kabisa ninavyo enda kulifanyia kazi haraka sana. Tulilala hapa, siku iliyofuata tuliamka hapa pamoja. Mpenzi wangu na mama Babuu walifanya kazΔ± zao huku na mimi nikiendelea kufuatilia kuhusu kile alicho nishauri.

Hakika ulikuwa ushauri mzuri hata nikiwa chumbani nilielezea kwa kifupi kwa baba yangu.

Baba aliniambia kwa upole β€œmwanangu ni kitu kizuri sana. Hakikisha huongei na mtu mwingine ambaye mnafanya biashara sawa kuhusu mawazo yako. Kwasababu anaweza kufanya kabla yako ukabaki unashangaa.

Kwenye maisha yako yote chunga mdomo wako kuongea vitu kabla havijatimia hiyo inaweza chelewesha au visitokee kabisa. Watu wanatakiwa waone tu umefanya. Hili ni wazo kubwa sana, mwanangu utakuwa tajiri sana nakuona mbali.

Mimi nipo na ninyi wanangu, kwa chochote kile nipo nanyo, Hata hivyo inatakiwa tuonane eneh niambie inakuaje?”
Nilitabasamu na kusema β€œmimi nipo nyumbani na mkweo, utakuja?”

Baba alisema β€œIla sio na mama yako, maana ananikera tu.”
Nilicheka na kusema β€œkaribu sana baba Tuna mengi sana ya kuzungumza.”
Baba alisema β€œleo sina kazi, nakuja kijana wangu. Sio muda dereva atanileta hapo.”

Başı mimi nilitoka nje kabisa, niliwaacha tu wao waendelee na mambo yao. Hivi unajua haoni lakini anafanya kazi zote za nyumbani.

Na sasa mimi sifuliwi tena na mama Babuu baby wangu ananifulia, anatandika kitanda vizuri hapo utaweza kuona hadi mwili unatumika kuhakikisha kitanda kinapendeza kwa kuchomekea shuka pembeni. Ni mwanamke msafi na mchapakazi.

Baba yangu alifika kweli, alinitazama na kusema β€œkijana wangu una nenepa.”
Nilicheka nikisema β€œbaba umeanza hivyo unajua.”

Başı tulicheka sana, niliongea naye kuhusu biashara, kuhusu namna leo nimefanya utafiti na mambo Kama haya. Tulizungumza kuhusu mtaji wake na gharama za kuanzia.

Zilikuwa ni pesa nyingi sana lakini baba aliniambia ukiwa tayari niambie lazima nikuchangie na wewe utajua mbele cha kufanya.

Nilimfurahia sana baba yangu, nilimwambia β€œbaba wewe ni mtu sahibi sana kwa maisha yangu. Nafurahia sana kuwa na baba Kama wewe. Nakupenda sana baba yangu.”

Baba alisema β€œninaye kijana mmoja tu, ambaye ni wewe unataka nifanye nini mwanangu.”

Nilitabasamu tu Kisha nilimwambia baba yangu β€œbaba nawaza kununua eneo lingine kabla ya kumuoa Pina. Sitaki Pina aje kuishi hapa kabisa. Kwasababu ya maisha niliyoishi na Gabby. Natamani Pina apate anacho stahili ni mwanamke mzuri sana. Sitaki kumkosa kabisa.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

SIMULIZI YA INGIZA FULL

NILIMPENDA KUPITA KIASI FULL

BIOLOGY TEACHER FULL