LOML | Love Of My Life (245)

 

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️: 245
Bibi alikuwa anatabasamu tu, Şam alikuwa na furaha sana lakini Pina muda wote ni kama amepigwa na butwaa. Bibi na Sam niliwafungulia mlango wa gari. Nilibaki na Pina nje na kusema “hutaki Sam awe mwanangu?”

Pina alinitazama na kusema “ni mama gani hana ndoto ya kuwa na mtoto na mwanaume Kama wewe Ricky. Wewe ni baba mzuri sana. Lakini lakini..”

Nikamuuliza kWa upole “lakini nini Pina!!, unahisi sitaweza. Nisamehe sana, nimesema Nakupenda, Nakupenda wewe na kıla chako, na watu wako. Şam ni mtoto wetu, mimi na wewe na hata bibi ni bibi yangu wewe tafuta bibi yako.”

Alicheka akilia kwa furaha na kunikumbatia akisema “Naishi maombi niliyoyaomba kwa miaka minne. Answered prayers, nashukuru Mungu.”

Nikatabasamu na kusema “haya Mama Şam tuondoke.”
Alitabasamu na kuniambia “Sawa baba Sam!!”
Unaweza kuona kila kitu ni utani, lakini kila tulichofanya ulikuwa ni upendo na kilifurahisha sana. Sisi tulifurahia sana.Ukiona bibi na Şam sasa wamefurahi sana.

Nilikuwa nafurahia sana hata namuuliza Şam, unapenda nyimbo gani, basi akitaja naweka, anafurahi sana akisema “baba kumbe kwenye garı kuna radio.”
Tunacheka sana, tunajikuta Tuna nyakati za furaha pamoja.

Tulifika mpaka nyumbani, mimi nilikuwa na Şam namwambia “Karibu sana nyumbani.”
Şam anashangaa anasema “nyumba yote hii, ni pazuri sana.”

Bibi na Pina na wao wanazungumza yao, baadaye niliwafuata wote ili tuingie ndani pamoja. Walipapenda sana nyumbani na mimi nili wakaribisha kwa upendo sana. Başı pamoja tulipata chakula.

Mama Babuu alifurahia sana kumuona bibi na Şam.Mimi na Şam tulielewana sana siku hii tulicheka, tulicheza na kufurahi pamoja.

Ni ndoto yangu kuwa na Familia kubwa na nzuri, Mungu amenipa familia, ninayo familia kubwa na nzuri tayari. Bado tu wa kutoka kwenye kiuno changu. Na nina mwamini Mungu mambo yatakuwa sawa kabisa.

Na Baada ya yote jioni niliwarudisha nyumbani kwao kwa furaha. Huku Pina akiniambia “nashukuru sana Mpenzi tumekuwa na siku nzuri sana. Mimi na bibi na Şam tumefurahia sana.”

Bibi alishukuru tena kwa kıla kitu akitamba namna amependeza huku Şam akiniuliza “baba Kwahiyo utatufuata lini tena tukacheze wote.”
Nilimuuliza “umependa eenh!!”

Aliniambia kWa furaha “sana.”
Başı nilichuchumaa na kusema “wakati ujao nitakupeleka sehemu maalumu ya michezo ya watoto. Utapenda sana.”
Şam alinikumbatia akisema “Asante sana, nafurahi sana.”

Ninashindwa kabisa namna ya kuelezea haya mahusiano yetu kwa namna ya kukufanya wewe uelewe kuwa kila kitu kilikuwa sawa kabisa.

Ni mwanamke mchapakazi, alikuja kwangu bila hata kuniambia wakati mwingine alifanya chochote kitu cha kunipatia furaha. Mpenzi wangu alikuwa zaidi ya mpenzi ni rafiki na zaidi.

Ndani ya miezi minne tangu niachane na Gabby, Hakuna hata siku nimewahi kujuta kuachana naye, Hakuna siku nimewahi kujuta kumfahamu Pina. Nilifanikiwa kWa mambo mengi sana.

Nilifanikiwa kibiashara maana hata mawazo ya Pina nilifanyia kazi. Biashara zilikuwa zinaenda kwa kasi sana. Rafiki yangu alikuwa anashangaa namna nilivyo tumia akili kwenye haya mambo. Başı na mimi nilimuelezea kuwa mke wangu ndiyo mwenye haya mawazo.

Alinishangaa sana huku akisema “una mke mwenye malengo makubwa sana.”

 

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata