
LOML | Love Of My Life (246)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️: 246
Nilitabasamu na kusema “kuna wazo lingine tena, hili nilisema litakuwa kwaajili ya rafiki yangu Kama atapenda mambo ya vifaa vya kisasa vya ujenzi.”
Willy alitabasamu na kusema “Ni wazo zuri lakini kwasasa pesa za mtaji sina. Subiri nijichange kisha tutaona.”
Nilimwambia kwa upendo “Ni sawa kaka, wewe ukiwa tayari mimi nakuazima na kisha utarudisha taratibu. Tumetoka mbali natamani tufanikiwe pamoja.”
Alinitazama akisema “ndiyo maana unafanikiwa kaka, lakini nisamehe mimi siwezi kuchukua hiyo pesa. Ila kaka naweza kufanya kitu kingine ambayo haiitaji pesa nyingi hivyo. Na unajua kabisa mimi kusimamia biashara sio mzuri kivile.”
Nilitabasamu nikisema “vyovyote tu. Ukihitaji mkono wa ndugu yako Usiogope niambie.
Nikiwa na baba yangu, alinipitia ofisini, akanielezea kuhusu eneo nilifurahi sana na pamoja tulienda na huu ndiyo wakati Pina wangu alianza kuhudhuria Clinic yake ya macho.
Tulifika mpaka kwenye eneo, lilikuwa ni eneo kubwa sana na eneo zuri sana. Sikutaka hata kupoteza muda kwani wenye nalo walikuwa wanashida sana, walikuwa wana pauza kwasababu wana uhitaji.
Baada ya makubaliano, na wahusika na watu wa serikali nilinunua eneo na siku hii hiii mambo muhimu yalifanyika huku nikiweka msisitizo kuwa natakiwa kujenga haraka sana.
Tuliondoka nikiwa na furaha sana, sikuwa naamini kuwa naweza kuyafanya haya mambo kwa nguvu zangu kwa umri ambao nilikuwa nao maana kila kitu baba alikuwa anatia nguvu. Nilifurahi sana hata baba alikuwa ananitania na tunacheka tu.
Siku moja wakati nimetoka kumchukua Pina hospitali nilimwambia kuwa ninayo zawadi yake na nataka akaone. Pina aliniuliza “zawadi gani teba hiyo mpenzi.”
Nilitabasamu na kusema “utajua tu!!”
Akaniuliza “Sasa baby nitaona vipi na sina macho?”
Nilitabasamu na kusema “Utaona kwa Hisia Pina mpenzi. Wewe una penda sana vitu vizuri. Na hiki ni matokeo ya mawazo yako unayonipa, akili unayotumia kunishauri, maombi yako na kıla kitu kizuri.”
Pina alitabasamu na kusema “looo!!, mwanaume una shukrani jamani mpaka raha.”
Nikamuuliza “una kumbuka daktari alichosema lakini?”
Pina alitabasamu tena na kusema “Pina huu ni muujiza, wala haionekani kama ni tatizo Kübwa sana. Utatumia dawa kWa kipindi chote ambacho tunasubiri hao madaktari na kisha tutawasikia wanasemaje, uhakika wa kuona ni 70/30. Endelea kumuomba Mungu.”
Nilicheka na kusema “umeamua uongee kama daktari sasa. Naimani unatumia dawa vizuri, hivyo siku ukiona utaona vingi sana.”
Alicheka na mimi Nilitabasamu tu.
Nilifika mpaka eneo hilo, nimshusha mpenzi wangu na kumwambia maeneo tulipo na kisha alisema “tumekuja kufanya nini mpenzi?”
Nilitabasamu na kusema “Hapa ni eneo letu, hapa tutajenga familia yetu pamoja. Mpenzi endelea kuomba tupate mvua ya wateja, tupate mvua ya mafanikio ili tujenge mafanikio haya pamoja. Nakupenda sana Pina.”
Pina alitabasamu huku machozi ya furaha yakimtoka na kusema “huu ni uwanja si ndiyo?”
Nikamwambia nikitabasamu “sio uwanja ni uwanja wetu, mimi, sam na wewe tutaishi hapa.”
Alinikumbatia huku akili ana kusema “Mungu wangu wa Mbinguni, unafanya zaidi ya nilivyo Omba. Asante sana Mungu kwaajili ya yote yanayotupa. Mbariki baba huyu, Mbariki kıla eneo La maisha yake. Bariki moyo na kazi zake. Nilindie sana maana yeye ndiye msaada pekee. Nakupenda sana mpenzi.”
Nilitabasamu na kusema “Nakupenda sana Mke wangu mzuri. Asante kwa kuja kubadilisha maisha yangu na kunionesha maana halisi ya upendo wa mke na mume na kunihakikishia kuwa kuna wanawake wazuri sana wapo na ukitulia naye unafanya maisha safi kabisa.
Başı haoni lakini namna anatembea huku na kule, alifanya hiki na kile mimi nilikuwa namchukua video na kumpiga picha tu huku nacheka. Başı alianza kuomba kibali na ulinzi na mafanikio kwenye hili eneo.
Nilikuwa natabasamu vile nimepata zangu mwanamke wa Mithali. Nilimchukua matukio ya mambo mengi sana. Alipomaliza niliomba nimrudishe nyumbani.

