
LOML | Love Of My Life (247)

๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ: 247
Hapa sahau kuhusu Pina wa zamani, Pina wa sasa ni mzuri zaidi, anawaka, na vile tunapaka mafuta mazuri utatuambia nini. Tumependeza mno, ni mwanamke wa hadhi yangu kabisa.
Niliendesha gari mpaka nyumbani kwao Pina. Hapa sio kama zamani. Ingawa Pina Mara nyingi nakuwa naye kwangu lakini hasahau kwao. Nilifanya marekebisho makubwa kupaka rangi, kuweka tiles mpya na kuwabadilishia madirisha.
Na vitu vya ndani kwa namna niliweza. Nje nikawajengea jiko na mahitaji yote muhimu ili mradi tu wajisikie vizuri kuwa hapo.
ลam na yeye ni shule na nalipia vizuri kabisa bila wasiwasi kabisa na anafurahia maisha yake ya shule mpya. Kiufupi nilitamani hata kama sio sana basi walau maisha ninayoishi mimi na wao waishi hata kidogo tu.
Pina alifurahia sana, tuliagana na nilirudi nyumbani. Baลฤฑ nakumbuka nilipofika nyumbani simu yangu iliita, alikuwa ni mama yangu. Nilipokea na kumsalimia mama.
Mama yangu aliniambia โmwanangu, sikuelewi unajua. Ina maana ndiyo huyo kipofu wako amekukataza hata kuzungumza na mimi. Nasikia umenunua eneo hunambii chochote. Hivi una shida gani wewe?โ
Nilijikaza sana, nilitamani hata nisimjibu kabisa nilishindwa, nilimjibu mama yangu โMama, unanikera sana, sikuhizi una roho mbaya sana.โ
Halafu nilikata simu.
Hapo ujumbe uliingia โunanikatia simu kisa kumwambia ukweli mwanangu. Umekua vibaya au sio.โ
Nilichukua ule ujumbe na kumtumia baba yangu. Baba alipiga muda uleule na kusema โkumekucha ni nini tena?โ
Nilimwambia baba kWa hasira โSijui mama ana tatizo gani, hawezi kumuongelea Pina kwa mazuri. Kฤฑla akipiga lazima tugombane. Baba mimi ni mtu mzima, nachoka sasa, nitapoteza uvumilivu kabisa kwake. โ
Baba alisema kwa upole โpole sana mwanangu, Pole sana. Nakuomba usiendelee kugombana naye mimi nitazingumza naye na kฤฑla kitu kitakuwa sawa kabisa.โ
Nilisema kWa upole โfanya hivyo baba, mimi nachoka, nashindwa kuvumilia kunitukania mwanamke wangu na kumsema vibaya kฤฑla akipata nafasi ya kuzungumza na mimi. Mama ana kera sana.โ
Nilikata simu, hata furaha yangu mama anataka tu kunikwaza ili mradi. Nashukuru ninaye baba yeye ananituliza sana.
Mama utadhani alizaliwa na utajiri, anakuwa sio muelewa kuwa hata yeye kesho na kesho kutwa kilichompata Pina kinaweza nipata hata mimi.
Anapata wapi ujasiri wa kuwa na roho ngumu namna hii. Ni mama yangu lakini sikupenda kabisa tabia yake kwa mwanamke wangu ambaye mimi ninampenda sana.
Nakumbuka siku mbili baadaye nilitembelewa na mgeni ofisini kwangu. Alikuwa ni mume wa Giana.
Nilimkaribisha, na yeye aliniambia โkaka nipo hapa kukushukuru kwa upendo wako, kwa hekima na kuokoa ndoa yangu. Nilikuwa sio kijana mzuri kwa mke wangu, pengine ulichokiona ni kidogo sana.
Lakini Kiukweli nilikuwa nipo vibaya zaidi. Baada ya yale maneno siku ile nilitafakari sana na kujiuliza ninakosa nini nikitulia na mke wangu na kutunza familia yangu.
Niliacha kabisa habari za kuruka huku na kule. Nilipata muda wa kukaa na kuzungumza na mke wangu. Tuliamua kufanya maisha yetu kuwa mazuri.
Tangu hapo kaka, Mungu ametubariki sana, maisha yamekuwa rahisi kuliko awali. Wewe ni kama Malaika alikutumia kuja kuniamsha usingizini. Ni kama nilipitia yale nifahamiane na wewe.

