
LOML | Love Of My Life (248)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️: 248
Maisha yangu yana mafanikio sana kaka, nakushukuru sana. Mimi na mke wangu tunakushukuru. Nilijisikia vibaya baada ya kujua uliachaana na mke wako, lakini sikushangai wala sitakulaumu.
Ninakuombea heri ukutane na mwanamke mzuri wa maisha yako. Mimi na familia yangu tuna shukuru sana.”
Nilitabasamu na kusema “Nashukuru sana kaka, Giana anaendeleaje?”
Alitabasamu na kusema “ni mke mzuri sana kwangu, Tuna furaha sana. Anakusalimia sana. Ilikuwa tuje pamoja ili ameshindwa kuna mambo yameingiliana.”
Mimi moyoni najua ni kwasababu ya lile tukio bado anaona aibu. Lakini kama ameamua kubadilika na kumrudia Mungu mimi ni nani nimuhukumu.
Nilimwambia huyu mwanaume Mwenzangu “hongera sana, msalimie sana Giana na mtoto. Mwambie awe na amani sana na ninawaombea mzidi kuwa na furaha.”
Wakati naongea hivyo, Mara nilisikia mlangoni Pina anaingia akisema “Loml, Unaendeleaje?”
Haraka niliinuka na kumpokea maana alikuwa na fimbo. Alipoingia alisema akideka “Ooh baby samahani, sikujua una mgeni hapa.”
Nilitabasamu na kusema “Relax mpenzi, huyu ni rafiki yangu mwingine hatujaonana muda mrefu sana. Unamkumbuka Giana, Gabby’s best friend?”
Aliniambia “Yes!!, nakumbuka, nakumbuka.”
Nikatabasamu na kusema “mume wake, amepita kunisalimia.”
Pina alitabasamu na kusema “Karibu sana, ni matumaini yangu mpo salama.”
Nilitabasamu na kumtazama mume wa Gina vile ananishangaa na kumtazama Pina anatabasamu. Pina ni mzuri sana anavutia halafu hana kiburi wala dharau.Nilisema “bro, anaitwa Pina, Love of my Life, ninampenda sana.”
Alitabasamu na kusema “mnapendeza sana, ninayo furaha sana kwaajili yenu.”
Başı Pina alisema “mpenzi, nina njaa, nakaa hapa nje nasubiri mmalize tukale au unasemaje?”
Mimi nilitabasamu tu huku huyu mume wa Giana akisema “sina hata sababu ya kuendelea kukaa. Pina mwanaume wako ni mzuri sana, ni mtu mzuri sana. Unatakiwa kumtunza na kumjali. Ana roho nzuri na safi sana.
Pengine watu hawasemi sana kuhusu yeye. Ila tunampenda. Kaka Hongera sana, mnaendana, ni mzuri sana, ni mzuri mno. Mimi naenda sasa.”
Sisi tulitabasamu tu, alitoka na Pina alisema “Napenda the way you make peace with everyone aliyekukera wakati ule.”
Nilitabasamu na kusema “tunasamehe halafu hatuwi washikaji tena ni kule na mimi kuleeee. Nimejifunza kuwa wengine wanaomba msamaha ili akuumize tena, mwingine sio kwamba anajutia Ila tu anataka amani ya moyo wake, na mwingine ili aendelee kupata alichokuwa anapata kwako. Sasa hivi Nimejifunza, I need no one around. Ninaye Pina ananitosha.”
Tulitabasamu na kupigana busu tu. Kisha tulitoka pamoja na kwenda kula. Kwa ufupi maisha yalikuwa ni mazuri sana.
Pamoja kwa furaha tulitoka, na Vile Pina mchangamfu kila mtu alimzoea pale ofisini. Na no dereva alimpeleka hospitali na kumsubiri. Mwanamke wangu msafi anapendeza sana. Nina mfurahia.
Tulienda tulikula pamoja, mimi nikarudi ofisini na yeye alienda zake kwao. Ijumaa au alhamisi ndiyo alikuja kwangu na kukaa mpaka jumatatu au jumanne tulizoea hivyo na kıla sıku namuona mpya, kıla siku nazidi kumpenda sana.
Siku za weekend tulienda sehemu za kufurahia na Şam na baada ya hapo dereva ana mrudisha nyumbani mimi nabaki na Pina wangu, cha madeko wangu. Tunafurahia maisha, namtembeza huku na kule bila kujali hata haoni mimi nafurahia kuwa naye.
Siku zilisogea, maisha yalienda. Kusema ukweli kıla kitu kilikuwa ni kizuri na hata ujenzi ulianza. Ujenzi pesa ikiwepo huenda haraka sana kıla baada ya wiki mbili tulienda huko kuangalia nikiwa na mpenzi wangu au mpenzi wangu na baba yangu.
Niliona raha kumshirikisha mpenzi wangu kila kitu changu kwasababu changu ni chake ninachotumia atatumia.
Maisha hayakuwa na kelele, mama nilikaa naye mbali huku tukiomba afungue moyo wake na kuondoa hasıra na chuki alizojaza ndani ya moyo wake kwa mtu ambaye amfahamu na wala hajawahi kuwa na tatizo kwenye maisha yake.
Kiukweli kabisa, sikuwahi kusikia wala kufuatilia habari za Gabby, wapenzi wake na nini anafanya niliamua kujiweka mbali na yeye na familia yake wapambane kama ninavyo pambana na mama yangu. Siku moja nikiwa ofisini nilipokea ujumbe kutoka kwa namba ngeni.Nilipofungua ndiyo nilijua ni Nani.

