LOML | Love Of My Life (249)

๐‹๐Ž๐Œ๐‹ (๐‘ณ๐’๐’—๐’† ๐’๐’‡ ๐’Ž๐’š ๐’๐’Š๐’‡๐’†) โฃ๏ธ: 249
Alikuwa ni Gabby. Aliniandikia ujumbe huu โ€œRodricky, sipo hapa kukukwaza. Nipo hapa kuomba msamaha wa dhati kutoka moyoni mwangu. Ninafahamu huniamini tena, hunipendi, hunifikiriii, wala hutaki kuniona.

Ninakuelewa kwasababu hakuna binadamu anaweza kuvumilia yale nimekutendea hata mimi mwenyewe ningetendewa nisingeweza. Wewe ni mwanaume wa pekee sana Ricky.

Nipo hapa kusema nisamehe sana, nimekosa kutoka moyoni nahitaji msamaha wako. Kila kitu kwangu ni kibaya. Familia hainipendi tena wala hawana imani na mimi kama zamani ingawa nimetafutiwa watu mbalimbali wa kuzungumza nao na nakiri ni kweli naendelea vizuri.

Ricky nashukuru umenifanya nijitambue, nijue thamani yangu, sikuwa najua kujipenda ni pamoja na kuupa thamani kubwa mwili wangu kuanzia ndani mpaka nje. Ninaumia sana kukukosa, wewe ndiyo kitu pekee nakosa kwenye maisha yangu.

Asante Umenifanya nibadilike sana, nimemrudia Mungu Ricky na naelewa neno lake. Najua hunitaki Tena, lakini Mungu hajaacha kufanya muujiza bado naimani wewe ni wangu. Namuonea wivu sana huyo mwanamke uliye naye.

Sijui amefanya nini kukupata wewe. Najua hawezi kukuacha kwa urahisi kwasababu wewe ni ndoto ya kila mwanamke. Ricky mimi nakupenda sana, mimi nakupenda kweli, mimi nakupenda kuliko yeyote.

Hakuna mwanamke anaweza kukupenda zaidi yangu.Ni mimi hapa mke wako, kwangu kufuta kuwa tumeachana ni ngumu sana. Ricky nateseka, naisha tu mwili wangu kila nikikuwaza, sina nuru, Sina maisha tena kama zamani kukukosa wewe ni kukosa kila kitu.

Nakuombea sana, nakuombea mno. Nasikia unafanikiwa sana, nakufuatilia mtandaoni kwenye kurasa za biashara natamani ujue ni machozi kiasi gani nalia. Nakupenda Ricky, Nakuombea, na naamini utanisamehe siku moja.

Nisamehe kWa ujumbe hii wenye read more, ni kwasababu nimeshindwa kujizuia nimekukumbuka sana, I miss you Bedo๐Ÿ˜ญ๐Ÿ’”, alikuwa sahihi yule mwanamke aliniambia NIMEPOTEZA, kweli kabisa nimepoteza.

Nilikuwa mjinga sana, nilikuwa mpumbavu sana, nilijua huwezi kuniacha kwasababu ya uzuri wangu na urembo wangu Kumbe kila mtu anao uzuri wake. Na mambo mengi yanapita kasoro upendo.

Ndoa yangu kuipoteza ni Kama sipo duniani, nahisi kuchekwa na kila mtu. Nimepoteza marafiki na kila mtu. Kwasababu tu sina upendo wako. I miss you Dadie๐Ÿ’”๐Ÿ˜ญ, Nakupendaโฃ๏ธ, sana, Nakupendaโฃ๏ธ.

Sikutaka hata kumjibu huu ujumbe, nilifuta meseji haraka sana. Na wakati nafuta iliingia picha. Nilitazama na kujikuta nacheka tu.Gabby sijui ameokoka zake kanisa gani baลŸฤฑ analia kanisani kakumbatia Biblia.

Ni kweli kapungua Ila mimi wala hanishtui kabisa maana hata kama anabadilika abadilike kwaajili yake na maisha yake sio kwaajili yangu. Nilifuta tu wala sikujibu asije nigombanisha na Pina wangu kisa upuuzi wake.

Niliendelea na maisha yangu, nyumba nayo ilizidi kusonga. Mama yangu tuliwasiliana Ila sio kwa upendo kabisa ni kama kuna kitu ananitafuta.

Nakumbuka biashara nazo namna zilikuwa zinafanikiwa. Willy alikuwa mtu muhimu sana. Mke wake na Pina wakaelewana pia.

Tulikuwa tuna tamaduni za kutembeleana ili kudumisha undugu wetu.Maendelo yake clinic ya macho yalikuwa mazuri na sasa tulikuwa tunasubiri hao mabingwa waje tuone upasuaji unakwenda vipi.

Siku moja nilikuwa nyumbani mama yangu alinipigia kujua nilipo nami nilimwambia nipo nyumbani. Aliniambia anakuja nyumbani kuna mahali ametoka ni jirani na hapa kwangu basi nilimkaribisha.

Kweli mama alifika Ila hakuwa peke yake alikuwa na binti umri wetu tu huu huu kama Pina au mdogo kidogo kwa Pina. Baada ya kufika mimi niliwakaribisha.

Mama akawa na furaha sana akisema โ€œbaba yako amenionesha mjengo wako Kwahiyo unanificha namna hiyo mwanangu hutaki nikaone?โ€
Nilimwambia kWa upole โ€œsio hivyo mama una ratiba nyingi tunapishana ndiyo maana.โ€

Mama alisema โ€œhalafu sijakutambulisha, anaitwa Vanessa, Ni mtoto wa rafiki yangu sana. Walikuwa Arusha wamehamia Dar ni wageni. Kama hutojali mnaweza kuwa marafiki umtembezetembeze.โ€

Nilitabasamu tu, najua akili ya mama yangu, nilisema โ€œnashukuru kukufahamu Vannesa. Karibu sana Dar es salaam. Ni mji ambao hata ukiamua kuzunguka mwenyewe unaweza kwasababu kila kitu kipo wazi kabisa. Mimi ratiba zangu ni ngumu kidogo mama anajua.โ€

Vannesa na mama walitazamana, huyo Vannesa sasa kama Gabby tu vizungu vingi na mapozi kibao. Mama aliniambia โ€œmwanangu bado hujaoa unaweza jikuta Mungu amekuletea mke kupitia anama yako.โ€

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

BIOLOGY TEACHER FULL

SIMULIZI YA INGIZA FULL

LOML | Love Of My Life FULL

SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? FULL