
LOML | Love Of My Life (252)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️: 253
Nilitabasamu na kusema “nataka tu marafiki wachache, wafanyakazi wangu, baba yangu na mama ingawa sina hakika kama atakuwepo basi na familia yake.”
Tulifurahi na hata tulianza tafuta kurasa za Pete nzuri. Nakumbuka sana.
Nilikuwa na mambo mengi nisimamie kazi, niende Site nitafute nguo nzuri kwaajili yangu na mtoto Sam na bibi na zaidi ya yote mpenzi wangu nguo ya kuendana na tukio maalumu La Ijumaa.
Siku ya jumanne ndiyo nilimwambia baba na nilimuomba baba azungumze na mama ili mama pia afike pale. Jumatano baba alinipigia kunipongeza na kusema kila kitu kipo sawa.
Nilitafuta hotel, nikalipia ili waandae kila kitu kwaajili ya mpenzi wangu. Na siku ya alhamisi mpenzi wangu alikuja nyumbani. Kama kawaida nikiwa naye ni furaha sana.
Haswa nikitoka kazini namkuta nyumbani unajua tena unachangamsha damu na mnacheza cheza başı burudani. Siku ya Ijumaa sasa asubuhi niliamka, na mpenzi wangu aliamka.
Nilisalimiana naye kwa upendo nikitaka aniambie jambo lake alicheka akisema “Subira ya vuta heri. Muda utakao niambia kuhusu jambo lako ndiyo nami nitasema.”
Nilitabasamu nikisema “nina hamu sana, nina hamu sana. Sasa kuna mambo naenda shughulikia. Mchana sitakula, Ila jioni msipike nitawatoa.”
Alitabasamu na kusema “Nakupenda sana mume wangu.”
Nilitabasamu na kusema “Nakupenda sana mke wangu kipenzi.”
Nilikumbatiana naye na kusema “nakupenda sana Pina.”
Alicheka na kusema “nina hamu sana na kesho. Nataka kukuona na hii sura yako nzuri.”
Nilitabasamu na kusema “nitakufuata saa moja.”
Alisema akitabasamu “muda wote utakuwa busy jamani kwani unafanya nini.”
Nilisema nikitabasamu “Tulia mchumba , tulia.”
Başı nilitoka zangu, nikaenda kwa bibi Nikamuelezea na nilimuomba asiseme chochote kile. Bibi alijawa na furaha sana. Na mimi nilifurahi.
Nilikumbatiana na bibi, nikampa mfuko wake na nilimwambia dereva saa 12 anawafuata aoge Ila hizi nguo abebe atavaa akiwa saluni. Bibi alifurahi sana.
Nilienda mpaka hotel, Willy alinisadia kuweka mambo sawa maandalizi yalikuwa moto sana. Sasa muda nao ulikuwa unaenda kasi. Lakini kila kitu kilikuwa safi kabisa. Pale Hotel sehemu ya kufanyia jambo langu ilipambwa vizuri na picha zetu, na furaha zetu. Hakika palipendeza sana.
Nilipokuwa hotel nakagua Mara ya mwisho ili sasa nikajiandae. Simu yangu iliita. Alikuwa ni mama Babuuu, nilishangaa kuona simu yake na kujisemea “sijui anataka nini tena.”
Willy yeye alikuwa tu na mambo yake. Başı nilipokea simu na nilisikia mama Babuu akisema “Upo wapi?”
Nilitazama simu nijue ni yeye au Nani inakuaje ananiuliza nilipo, nikamuuliza “una nini?”
Mama Babuu aliniambia “mama yako yupo hapa, amemtolea maneno machafu sana Pina. Ameingia chumbani kwenu na kuanza kumfukuza. Nimejitahidi kuzuia sijaweza.
Amemtupia vitu nje na nilipo jaribu msaidia na kumfuata nje alinikaripia nirudi ndani. Sijui hata atakuwa kaenda wapi mbaya zaidi fimbo yake ninayo hapa.Na mama yako ameondoka.”
Nilikata simu haraka haraka na kuangalia kwa simu Camera za nyumbani. Nilianza kuangalia mama alipofika mama Babuu alikuwa na Pina jikoni. Pina alimkaribisha mama na kumsalimia.
Mama yangu alisema “maskini mkubwa wewe, huna kwenu, kukicha kwa mwanangu. Eti anakuvisha pete kWa kipi haswa. Sikupendi na kamwe huwezi kuwa binti yangu. Na hapa utaondoka.
Mabinti wengine bhana kuona mwanangu ana pesa una mganga angekuwa maskini ungeganda hapa.Na huo upofu wako unaona unapendwa sana.”
Natazama mpaka natetemeka, Pina machozi yalimtoka na kusema “mama sio wewe sio yeyote atakatisha mapenzi yangu na Ricky. Tunapendana sana. Mimi sijali kuhusu wewe kwasababu kijana wako ananipenda hata hivyo sijakukosea kitu.”
Mama yangu alimpiga kibao , nilifumba macho yangu vile Pina anaugulia na mama Babuu Ana saidia inashindikana, halafu alisema “una mdomo sana, ile siku hospitali nimekuacha unaona unaweza kunijibu unavyotaka maskini mkubwa wewe huna hadhi ya kuwa na mwanangu. Kijana wangu ataona tajiri mwenzake.”
Niliona mama yangu anamsukuma na kumvuta mwanamke wangu nje ya nyumban yangu. Anafoka vitu havieleweki.
Share kwa ndugu na marafiki
WhatsApp
Facebook
Twitter

