
LOML | Love Of My Life (257)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️: 257
Siku ya kurudi nyumbani ilikuwa ni siku ya furaha sana kwetu. Nyumba yangu ilichangamka sana. Huku wazazi, huku mke wangu kipenzi Pina na familia yake mama Babuu, marafiki zangu ni furaha tu. Pina alikuwa anafurahia dunia akisema “nilikumbuka kuona vitu vingi, dunia ni nzuri sana jamani.”
Wote tulicheka sana. Tulipika na kula pamoja.
Nakumbuka sikutaka kupoteza muda, baada ya kukaa sawa tu huku nyumba yangu inaendelea kujengwa mimi nilitangaza ndoa na Pina wangu. Sikutaka mimba yake iwe kubwa ndiyo tufunge ndoa.
Başı kwakuwa niliwahi kuoa sikutaka mambo mengi. Ndoa ilitangazwa na siku ya ndoa kwa furaha na wazazi wetu Pina sasa akiwa anaona kabisa tulifunga ndoa yetu nikimwambia mke wangu kipenzi “Loml wewe ni mwanamke pekee ambaye maisha yangu yote nataka nilale na kuamka nikifumbua macho yangu namuona yeye kila asubuhi.”
Pina alitabasamu na kusema “Nakupenda sana Hatima yangu, leo hii wewe ni mume wangu, wangu peke yangu. Nakupenda.”
Watu walifurahia sana.
Ilikuwa ni harusi ndogo lakini iliyokuwa na furaha kubwa na sasa Willy na mke wake ndiyo walitusimamia. Habari za ndoa yangu zilikuwa sehemu mbalimbali na tulifurahia lakini kitu kibaya kilitokea usiku huu wakati tunarudi nyumbani.
Hatukurudi nyumba ya zamani Bali nyumba mpya. Tulipofika tu, nilipokea simu ya Willy, aliniuliza “unaona yanayoendelea mtandaoni?”
Nikamuuliza “mambo gani tena na unajua mimi leo nilikuwa na shughuli.”
Ndipo alikata simu na kunitumia picha. Ni Gabby, Gabby alijinyonga na kuacha ujumbe ambao ulisambaa mtandaoni. Ulisomeka hivi “Maisha ni safari ndefu sana. Kusema kweli nimefanya makosa mengi sana lakini kosa kubwa nikumpoteza mwanaume wa maisha yangu.
Ninaumia sana, lakini siwezi kufuta niliyomkosea. Sikuwa mwanamke mzuri kwake. Ombi langu kwa wanawake Wenzangu ukipata ndoa mpende mume wako, muheshimu na umjali kwa hali na mali.
Leo hii mimi nimeishia hapa kwasababu nimekubali NIMEPOTEZA, nimepoteza matumaini yote. Nilitamani isiwe kweli, lakini sitaweza kuvumilia mwanamke mwingine na mume wangu ambaye ndiye mwanaume peke aliyewahi kunipenda.
Wazazi waleeni watoto katika njia sahihi, waficheni watoto na mahusiano yenu ya kila aina, sitamani muwape simu Ila najua mtaniona mjinga mengi nilijifunza huko na umri mdogo sana.
Acheni kulea watoto kimayai hata neno la Mungu linasema usimnyime mtoto mapigo. Haina maana umpige ovyo lakini ni wajibu kumkanya na kumlea katika njia impasayo Mungu.
Ricky najua leo umefunga ndoa, najua una hasıra na mimi, najua nimekuumiza, najua hunipendi kabisa pleaseeeeeeee, naomba uje kunizika, usinitelekeze nakuomba sana, nakuombaaa unisamehe kwa yoteee, sikuwa napenda kufanya nilikuwa nafanya baadaye najuta sana sijui hata nilikuwa na kitu gani kwenye maisha yangu.
Lakini pamoja na yote upendo wangu kwako ulikuwa wa kweli kabisa. Hongera umepata mtu wa kukufanana Nakutakia maisha marefu na mazuri. Ni mimi Bedo 💔😭.Mungu nisamehe , Mungu nihurumie mimi ni mjinga sana, sifai, sio mfano mzuri. Asante pia kwa kunitunzia aibu yangu. Nitakukumbuka milele kama kuna nafasi ya kukumbuka bado watu wazuri.Wewe peke yako ulinijali hata kwenye aibu baada ya hapo kila mtu ananikataa.”
Nilimuonea huruma sana kwa njia aliyochagua na hata nikamsimulia LOML kilichotokea. Alisikitika sana akisema “alikuwa bado anayo nafasi ya kujenga maisha yake. Kwanini amejinyonga lakini. Pole sana Mpenzi wala usisikie hatia. Amejiua yeye mwenyewe, hujaua wewe.”
Nilimkumbatia mke wangu na kusema “Nakupenda sana.”
Mke wangu alisema “tulale sasa kesho tukazike.”
Nilijikuta tu nakosa raha. Tulioga, tukapumzika.
Asubuhi tuliwasiliana familia tukaenda kumzika Gabby. Natamani angeona mama yake anavyolia, baba yake anavyoumia asingechukua maamuzi hayo magumu.
Msiba ulikuwa na watu wengi hata Mc nilimuona hapa. Sikujali mimi, baada ya kuzika nilienda kwa baba Gabby tulikumbatiana akanipa Hongera na kushukuru mimi kuwepo pale. Baada ya hapo mimi na familia yangu kwa masikitiko tulirudi nyumbani.
Kamwe kwenye maisha usiwaze kujiua. Ukijiua wewe watu kwa msiba wanaolia ni wachache sana wengi ni umbea na wanagombaniana mpaka chakula na ndani ya siku chache wanakusahau. Suluhu ni nyingi sana zaidi Kuna Mungu anayetatua hata magumu sana.
Niliishi na mke wangu, na mtoto Wangu Şam kwa upendo mkubwa sana na mama Babuu. Nilianza na kazi, mke wangu alilea mimba nikiwa naye bega kwa bega na alijifungua watoto wawili mapacha. Mama yangu alifurahi sana na alikuwa hapa na sisi kuhakikisha mambo yanakuwa sawa.
Mama na Pina wakawa marafiki wazuri sana na watoto hawa walileta baraka Şam sasa alipata dada mmoja na kaka mmoja. Tulifurahia sana. Maisha yalizidi kuwa Bora. Mke wangu sasa na yeye alianza kazi kwenye ofisi zetu wakati nyumba ile nimeipangisha.
Miaka mitano baadaye bibi aliugua na kufariki tulizika kwa masikitiko makubwa maana alikuwa mtu mzuri sana kwetu na tulimzoea sana. Tuliendelea na maisha yetu.
Tangu mke wangu kajifungua ilipita miaka 10 mke wangu alibeba mimba tena kwa uwezo wa Mungu. Muujiza juu ya muujiza. Unaweza sema kitu leo kwa Mungu ukaona utani kumbe Mungu ametick.
Nilisema nataka familia kubwa, ndiyo baada ya miaka kumi tulipata mapacha watatu wote wa kiume. Hivyo sasa nina watoto 6. Şam wa kwanza na watano wadogo zake.
Familia kubwa ya upendo mwingi sana na Mungu anatubariki maisha safi kabisa. Familia inayo mpenda Mungu na tunaishi vizuri sana tuliwalea watoto kwa njia impasayo Mungu nikiwa na LOML.
Unaweza ukawa unapitia maisha fulani huyaelewi. Ukawa unasali sana , unaomba sana bila mafanikio yoyote yale na ukafikiri Mungu amenyamaza. Mungu hajawahi kunyamaza kwenye Yohana 10:7 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.
Mungu anawajua walio wake, na walio wake wanaisikia sauti ya Mungu. Usichoke kuomba kuwa na uvumilivu mpaka Mungu atakapo kujibu. Usichukie kuwa nimefanya hivi imekuwa mbaya zaidi. Acha tu ilipaswa kuwa hivyo ili upatie. Msikilize Mungu.
Ukipata ndoa haijalishi ulikuwa Nani, ulifanya nini, heshimu ndoa yako hata kama ni mwanaume Hana kitu au mwanamke hana unavyopenda. Heshimu ndoa yako. Ndoa ni Mungu mwenyewe. Unaweza ukafanya ujinga wakati bado unahitaji ndoa yako na mwisho ukachelewa. Ndoa sio kuhusu mimi mzuri au nina pesa. Pindi mwenzako akichoka hatageuka nyuma tena atakutana na mzuri zaidi yako hapo ndiyo utajua Kumbe wewe hukua mpenzi wa maisha yake kabisa.
Mapenzi Au maisha sio kuhusu tajiri na maskini sisi wote tunategemeana ili uwe wewe lazima mimi niwepo na ili mimi niwe lazima wewe uwepo. Hakuna amri nzuri zaidi na kubwa kama upendo. Acha kudharau watu kisa muonekano au kipato chao.
Zaidi ya yote mzazi kuwa karibu na mtoto wako msome na ujue tabia zake furaha na huzuni zake msaidie kuvuka hapo. Kumlea kama yai sio malezi, kumuachia dada wa kazi hata ukiwa na nafasi utaharibu huyo mtoto mpende na mlee vyema.

