LOML | Love Of My Life (04)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:04
Niliendelea kumsaili huku moyoni nikisema β€œni mwanamke anayevutia sana, amenivutia, ni mzuri sana.”

Sijui hata kama unanielewa, nimetoka kanisani na kwa Mara ya kwanza naona kabisa nimekutana na love of my life (LOML). Sijamaliza hata kumtazama huyu mwanamke dereva naye alikuwa anaondoa gari.

Nilikuwa hata nainamia, nataka kumuona yule mwanamke mzuri. Lakini nashindwa, nilichukia, nilitamani tu nishuke ila nawezaje.

Sasa hapo G ananiambia β€œMine Ricky, upo ok?”

Nilimtazama, sio kwamba Gabriella ni mbaya, ana uzuri wake na si unajua mwenye pesa anajitunza vizuri ni mwanamke fulani hivi wa hadhi. Yule mwanamke ukimuona unajiuliza nimfuate au basi achana naye.

Ni mzuri ana jipenda sana. Lakinu sasa yule nimemuona ana uzuri wa asili na pale ndiyo maisha yake magumu. Ni kama malaika amenipa tu mwanamke siku ya ndoa yangu.

Aliniuliza tena akideka β€œRicky wangu. Please dadie, niambie are you happy?”
Nilijikuta nina furaha sana nikisema β€œvery happy, nina furaha sana G.”

G alitabasamu na kusema β€œnashukuru sana mume wangu, nakupenda sana mume wangu mzuri na asante kwa kukubali kuwa mume. Nakupenda.”
Nilimtazama na kusema β€œnakupenda mke wangu.”

Nilimkumbatia, lakini kumbato lote hili, akili yangu ipo kwa yule msichana ambaye hata jina lake silijui, lakini moyo wangu tayari umehisi uwepo wake, ni msichana wa aina yake.

Moyo wangu umemtambua na hisia zangu zimemwangukia, nahisi ninampenda sana yule mwanamke, mwanamke mgeni nisiye mjua na sijui hata wapi nitamuona tena.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata