
LOML | Love Of My Life (07)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:07
Nikiwa nimekaa namuwaza mpaka natabasamu, Gabriella aliniita βBaby, Husbae, njoo please!!β
Nikaitika nikisema βAm coming wifey!!β
Nasema hivyo mdomoni moyo hautaki, sijui hata unanielewa. Simuoni mke wangu tena kama ndiyo ninayepempenda, hayupo moyoni mwangu kabisa naona kero tu.
Sihisi kumpenda, nimegundua sasa kuwa mwanamke ambaye anaenda kuwa mke wangu wa maisha yangu yote mpaka kifo kitutenganishe sio mwanamke ambaye mimi ninampenda. Roho yangu imeumia sana, simpendi mke wangu, kuna mwanamke ambaye nimemuona ndiyo naona yeye ndiyo mapenzi yangu yote. Nitafanya nini sasa mimi.
Basi niliingia bafuni, mke wangu ni mrembo sana. Anavutia kila mwanaume ambaye ni rijali na atapita mbele yake lazima tu utakubali ni mzuri, ila ndiyo vijitabia vyake sasa mimi kwangu hapana mwingine kwake inaweza kuwa ndiyo na lingine ni kuwa tu moyo una macho na haujamuona yeye kama mke na sasa nimekutana na nini moyo wangu unataka natabasamu kila dakika kila muda bila kutaka mwenyewe.
Mke wangu, alinikumbatia kwa upendo, akanisogelea na kusema βbaby wangu, umechelewa. Nakusubiri kitandani mpenzi, leo mimi ni wako, wako peke yako, bila shaka tutakuwa na usiku mzuri sana.β
Kabla sijasema lolote alinibusu mdomoni.
Nilimtazama tu, simfurahii tena. Kuna mambo na vitu vingi sana, kuhusu mimi na yeye, lakini kiukweli kabisa moyo wangu haumuoni kama mke na hii mimba imefanya leo nipo fungate kwasababu wazazi wetu wametaka.
Nilioga, na baada ya kumaliza niliendelea kupoteza muda bafuni, nilipotoka sasa nikakuta mke wangu sasa amevalia nguo ya kulalia nzuri kabisa, amevalia vitu vizuri, anatabasamu, nilimtazama na kutabasamu nikisema βumependeza sana Gabby!!β
Alitabasamu na kusema βkwaajili yako Ricky wangu. Karibu.β