
LOML | Love Of My Life (100)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:100
Nilimtazama na kisha nilitoa wallet yangu na kuchomoa pesa nikasema βnauli hii hapa, mimi naelekea kazini. Tutaonana baadaye.β
Huyu mama alinitazama tu.
Mimi niliingia kwa gari na kuelekea kazini. Sikuwa na ile furaha ya kawaida unajua ile una muangalia tu mtu unajua huyu ana furaha. Sikuwa na hii furaha kabisa. Nilikuwa tu najilazimisha. Nilifika kazini kwangu, sio kazi ya familia ni kwangu mimi mwenyewe.
Nauza Ac na huduma ya kufungia wateja wangu majumbani, maofisini na mambo kama hayo. Ni ofisi kubwa kwa uwezo wangu ingawa na familia yangu nayo ina kazi zake. Napenda kujisimamia na ndiyo ipo hivyo tu.
Nilipofika tu kazini, msaidizi wangu alikuja ofisini kwangu, alinisalimia na kumuuliza kama kuna taarifa yoyote. Alinitazama na kusema βkuna barua hapa boss.β
Nilimtazama na kupokea ile barua.Kisha alitoka. Nilifungua ile barua alikuwa ni Max anaacha kazi. Nilisoma huku macho yanabadilika kuwa na rangi nyekundu. Nilikuwa nachukia, nilizidi kupata hasira.
Ni kama kaka, nimeishi naye vizuri yeye na mke wake na familia yake kwa ujumla. Nimemsaidia kwa mengi haitoshi kaona mke wake hatoshi na amekuja mpaka kwa mimi boss wake.
Huu mzunguko kwenye ndoa sijui utaisha namna gani ila kusema ukweli hili lilinikera sana nafsi yangu. Niliikunja ile barua kwa nguvu, nilijizuia nisifanye kitu kibaya ofisini hata nikalegeza vifungo vya shati langu maana nilikuwa najisikia vibaya sana.
Nikiwa katika hali ile rafiki yangu Willy alinipigia, na yeye ni anafanya kazi kama yangu lakini yeye hana biashara kubwa kama mimi na pia ameajiriwa mahali serikalini na maisha yake yanaenda vizuri.