LOML | Love Of My Life (101)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:101

Kwahiyo akipata dili kubwa na yeye hana mzigo anakuja kwangu, ananiunganisha mimi na kuna namna tunafidia hilo. Maisha yanaenda. Hivyo alinipigia na mimi nilimwambia ya kuwa nipo kazini.

Na yeye aliniambia kuhusu hao wateja na wanahitaji kwa haraka niwashughulikie. Nikamuuliza β€œina maana hutokuja?”
Akaniambia kwa upole β€œleo nimebanana ila nitapita hapo kaka.”
Nilitabasamu tu.

Basi nilianza kazi, kwakweli kampuni aliniunganisha nayo ni kubwa. Nilijipanga na team yangu na kushughulikia kila kitu. Ilikuwa ni nzuri sana. Kazi ilienda sawa na watu walikuwa wanafurahia. Mimi nikaendelea na mambo yangu.

Ilifika mpaka saa 6 hivi, bado nilikuwa ofisini. Kushika simu yangu, ina meseji za kutosha kutoka kwa mke wangu. Nilipofungua ni analalamika, anaomba msamaha.

Kuna moja aliniandikia β€œMpenzi, usiniache hivi, nitakufa mimi, nakuomba mume wangu, nakuomba mimi nipo tayari kufanya lolote lile ili mradi unisamehe. Nakuomba mume wangu.”

Nilishusha pumzi na simu yangu iliita.Alikuwa ni baba yangu. Nilipokea na kumsalimia baba yangu. Baba yangu aliniuliza β€œupo wapi kijana wangu?”
Nilimwambia baba yangu β€œnipo kazini baba.”

Baba alisikitika akisema β€œnilijua jana umenielewa mwanangu. Mtoto wa watu huyu, yupo hospitali. Kila mtu anajua kuwa mmepoteza mtoto. Na wewe haupo hapa baba yako nitajibu nini?”

Nilichoka na kusema β€œhata lini baba tutafanya mambo kwaajili ya kufurahisha watu wengine. Sio lazima mimi kuwepo hapo. Gabriella anajua alicho kifanya.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

BIOLOGY TEACHER FULL

BINTI MDUNGUAJI FULL

LOML | Love Of My Life FULL