
LOML | Love Of My Life (102)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:102
Baba yangu alisikitika na kusema βkwa heshima ya mimi baba yako, nakuomba.β
Nilishusha pumzi na kusema βNakuja baba, lakini ni kwaajili yako. Kwaajili yako.β
Baba alisema kwa huruma βnashukuru kijana wangu, asante sana.β
Nilikata simu na kuendelea na kazi kidogo, wakati najiandaa kutoka na rafiki yangu na yeye alifika. Basi nilimwambia kwa upole βmimi ndiyo najiandaa kwenda kwa mke wangu.β
Rafiki yangu alinitazama na kuniambia βlakini ni kama haupo sawa kabisa.β
Nilimtazama na kusema βni kweli kaka, sipo sawa hata kidogo lakini hili sio la kuzungumza sasa. Kwasababu sijui hata nianzie wapi. Ila nilikuwa sahihi, sikupaswa kumuoa Gabriella kwasababu ya mimba yake kwasababu hisia zangu zilikuwa zinakataa.
Nilisikiliza na kufuata ushauri wako, taratibu nilianza kuangukia kwenye penzi lake. Lakini Willy, daaah!!, mimi sijui kwasababu nashindwa kuongea ila kuna siku nitakuelezea, nitaongea na wewe. Utanielewa.β
Willy akanitazama na kusema βsasa kaka kama mambo ndiyo hivi sasa una raha gani na ndoa?. Kila siku unaona kama ulikosea kuoa, unaona humpendi mkeo, mtafika kweli?β
Nilimtazama na kisha nilisema βsijui kaka, tuondoke.β
Alinitazama na kusema βkaka, mimi nakuamini na kukutegemea sana. Usiniangushe.β
Niliinuka na kutabasamu na pamoja tulitoka. Safari ilikuwa hospitali, na tulitumia gari yangu na ya Willy ilibaki hapa.
Tulifika mpaka hospitali, Willy alisalimia familia haswa baba yangu na mama na kisha wazazi wa Mke wangu ambao hii siku walikuwa wamekaa pamoja ni wazi walikuwa na jambo wanaongea.
Kisha nilianza kuelekea kwa mke wangu bila kumsumbua yeyote. Tulipofika mlangoni tukasikia vicheko, inaonekana kulikuwa na watu ndani.
Taratibu nilifungua mlango, ni kweli kulikuwa na watu wengine sita akiwepo na Giana. Walikuwa wana furaha sana.
Ukiona Mke wangu sasa na alivyoniona alisema βbaby, karibu sana. Karibu mume wangu kipenzi.β