
LOML | Love Of My Life (104)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:104
Marafiki zake walikuwa wanafurahia hata wakaniaga kwa upendo na najua walikuwa wanatupa nafasi. Hata rafiki yangu aliniambia βutanikuta nje.β
Nilimtazama na kusema βnakuja sasa hivi.β
Alitoka na nilibaki mimi na mke wangu Gabriella tu. Sio kama sisi tuliokuwa tunacheka, uso umenibadilika na yeye analia.
Nikamuuliza βunafanya nini Gabby, unafanya nini?. Ni nani unayetaka kumuonesha una mahaba namna hiyo, ni nani ambaye unataka kumuaminisha nakupenda kiasi hiko?.
Kwanini usitambulishe wale wajinga wengine, sikia nikuambie, mimi msimamo wangu upo palepale, usirudi nyumbani, na sitaki kukuona nipo hapa kwasababu baba yangu ametaka niwepo hapa. Nakuchukia sana wewe mwanamke, nakuchukia.Fanya uache maigizo yako, unanielewa Gabby.β
Mke wangu alianza kulia akisema βmume wangu usifanye hivyo, tunahitaji kuokoa ndoa hii. Mimi na wewe pamoja, nipo tayari kufanya lolote ili wewe unipende tena.β
Nilimtazama na kusema βhivi unajua una drama sana wewe mwanamke, mimi sijui kwanini sikuwahi kuyaona haya kabla Mungu wangu ni nini hiki?β
Gabriella analia.
Na kisha hapo mama yake aliingia, nilimtazama nikawa nataka kutoka. Huyu mama aliniambia kwa upole βmwanangu, tunaweza kuzungumza?β
Nilimtazama na kushusha pumzi, huyu mama alinitazama na kusema βPleaseeee!!!.β
Nilimtazama tu huyu mama. Ni mama fulani hivi mzuri sana. Kwasasa mnawaita marich aunt. Anapendeza, eemh hata mama yangu na yeye unajua tena basi ni wamama fulani hivi wakupendeza.
Nilimuheshimu na kukubali ombi lake. Mama alimtazama mwanaye akamfuta machozi na kusema βmwanangu nitarudi.β